July 08, 2020

KATIBU WA BUNGE ATEMBELEA BANDA LA UTT AMIS KATIKA MAONESHO YA SABASABA 2020

Katibu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Stephen Kigaigai, akipata maelezo juu ya mifuko ya uwekezaji wa pamoja kutoka kwa Ofisa Uendeshaji Mkuu wa UTT AMIS, Josephine Mlimbila, alipotembelea banda la UTT AMIS katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (DITF).
 Baadhi ya wanachi wakipata maelezo kutoka kwa Ofisa Uwekezaji UTT AMIS, Fredrick Lushinge, kuhusu mifuko ya uwekezaji wa pamoja ya UTT AMIS walipotembelea banda la kampuni hiyo katika viwanja vya sabasaba.
 Baadhi ya wanachi wakipata maelezo kutoka kwa Ofisa Uwekezaji UTT AMIS, Fredrick Lushinge, kuhusu mifuko ya uwekezaji wa pamoja ya UTT AMIS walipotembelea banda la kampuni hiyo katika viwanja vya sabasaba.
 Naibu Kamishina wa TRA, Msafiri Mbibo, akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Masoko na Uhusiano Mkuu wa UTT AMIS, Martha Mashiku, kuhusu mifuko ya uwekezaji wa pamoja wakati alipotembelea banda la UTT AMIS katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (DITF). 
Baadhi ya wafanyakazi wa UTT AMIS wakiwa katika picha ya pamoja katika banda lao lililopo katika viwanja vya Sabasaba. 


Na Mwandishi Wetu

UTT AMIS ni kampuni ya serikali inayohusika na uanzishaji na uwendeshaji wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja. 

Pia wanatoa huduma za usimamizi wa mitaji binafsi (Wealth Management Services).

 UTT AMIS inatekeleza majukumu yake kulingana na sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya mwaka 1994 na marekebisho yake pamoja na kanuni za mifuko ya uwekezaji wa pamoja za mwaka 1997.

UTT AMIS kwa sasa inasimamia mifuko sita ya uwekezaji ambayo ni Umoja, Wekeza Maisha, Watoto, Jikimu, Ukwasi na Bond Fund.

Kwa Kuwekeza katika mifuko ya uwekezaji, wawekezaji wananufaika na unafuu wa gharama za uwekezaji, utaalamu wa uendeshaji kupitia meneja wa mfuko. 

Pia wawekezaji wanauwezo wa kufuatilia uwekezaji wao na kujua hali ya uwekezaji wao na soko kwa ujumla kwa urahisi kwani thamani ya vipande vya mifuko hutolewa kila siku ya kazi. Vilevile mifuko hufanya uwekezaji mseto katika dhamana mbalimbali sawa na sera ya uwekezaji ili kupunguza hatari za uwekezaji na kupata faida shindani.

Mifuko hii imeandaliwa ili kukidhi mahitaji ya wawekezaji wadogo na wakubwa huku tukizingatia malengo yao, muda wa kuwekeza, ukwasi,uwezo wa kuhimili changamoto uwekezaji na usalama.

Mathalani mfuko wa Umoja kiwango cha kuanza kuwekeza ni vipande 10 tu, sawa na wastani wa shilingi 6500. Mfuko wa Wekeza Maisha unatoa faida pacha za uwekezaji na bima ya maisha kwa kiwango cha chini cha shilingi 8340 iwapo mwekezaji atachagua mpango wa kuwekeza kila mwezi.

Mfuko wa watoto unalenga kuwawezesha wazazi kuanza kuwekeza mapema ili kukidhi mahitaji ya elimu ya watoto wao.Kiwango cha chini cha kuanza kuwekeza ni shilingi 10,000 tu. 

Mfuko wa Kujikimu unalengo la kukuza mtaji na kutoa gawio kila robo mwaka au kwa mwaka mara moja. Mpango wa robo mwaka kima cha chini cha kuwekeza ni shilingi milioni 2 tu na mpango wa mwaka kima cha chini cha kuanza kuwekeza ni shilingi milioni moja (1,000,000/-) tu.

Mfuko wa Ukwasi unalenga wawekezaji wa muda mfupi hadi mrefu wanaozingatia hatari ndogo za uwekezaji na urahisi wa ukwasi. Kiwango cha chini ca kuanza kuwekeza ni shilingi laki moja (100,000/-) na kiwango cha chini cha nyongeza ni shilingi elfu kumi (10,000/) tu. Pia Mfuko wa
Hatifungani( Bond Fund) unawekeza zaidi katika dhamana za serikali. 

Mfuko una mpango wa kukuza mtaji na mpango wa gawio. Mpango wa kukuza mtaji kiwango cha chini kuanza kuwekeza ni shilingi elfu 50 na mpango wa gawio kila mwezi kiwango cha chini kuanza kuwekeza ni shilingi milioni 10 na gawio kila baada ya miezi sita kiwango cha chini kuanzakuwekeza ni shilingi milioni 5.
 
Pamoja na kuwa na mifuko hii ya uwekezaji, UTT AMIS inatoa huduma binafsi ya usimamizi wa mitaji kwa mtu mmoja mmoja na kwa taasisi. Kupita huduma hii tunasikiliza hitaji mahsusi la mwekezaji na kumtengenezea mpango binafsi wa uwekezaji utakokidhi mahitaji yake. Kiwango cha chini cha kuanza kuwekeza katika mpango huu ni shilingi milioni 100.

Ukubwa wa rasimali za mifuko na faida ipatikanayo katika mifuko ni miongoni mwa vigezo katika kupima utendaji na ufanisi wa kampuni za uwekezaji. UTT AMIS imeendelea kutoa elimu ya uwekazaji na uelewa unaendelea kuongezeka.

Hadi kufikia Juni 30, 2020 jumla ya mali katika mifuko
ni zaidi ya bilioni 400. Pamoja na changamoto katika soko la hisa, thamani ya mifuko chini ya usimamizi wa UTT AMIS imeendelea kukua na kutoa faida shindani kwa wawekezaji na kuendana na maendeleo ya soko kwa ujumla.

UTT AMIS imeendelea kuwekeza katika mifumo ya tehama ili kuwezesha wawekezaji kuwekeza na kupata taarifa za uwekezaji kwa njia ya simu. 

Mifumo hii inafanya kazi kwa mwekezaji kupiga * 150*82# na kisha kufuata maelekezo. Pia kwa kuanzia mifumo ya UTT AMIS imeunganishwa na Mifumo ya benki ya CRDB ambayo pia ni msimamizi wa mifuko.

Hivyo, mwekezaji anaweza kununua vipande moja kwa moja kwa kutumia mifumo yote ya malipo ya benki ya CRDB.

UTT AMIS – Mshirika hakika katika Uwekezaji

No comments:

Post a Comment

Pages