July 13, 2020

Maziwa ya mgando yanasaidia kuimarisha kinga ya mwili


Mkurugenzi wa Kampuni ya  Specy Enterprise wazalishaji wa Maziwa ya Mtindi, Specioza Machume, akimuelezea mteja juu ya umuhimu wa maziwa hayo katika kujenga kinga ya mwili.
 


Na Mwandishi Wetu

IMEELEZWA kuwa utumiaji wa maziwa ya mngando ya Ng'ombe ni moja ya njia ya kusaidia kuimarisha kinga ya mwili na kuimarisha mifupa kwa wat wa rika lote.

Mkurugenzi wa Kampuni ya  Specy Enterprise wazalishaji wa Maziwa ya Mtindi,Specioza  Machume amesema watu wengi wanajua maziwa ya mgando hayasaidii kitu chochote ila ni moja ya kinga ya mwili.

Amesema wakati dunia inapokabiliwa na Changamoto ya ugonjwa wa Corona unywaji wa maziwa hayo kwa asilimia kubwa yanaweza yakasaidia kuimarisha kinga za watu kukabiliana na ugonjwa huo.

"Bidhaa hizi za Probiotic Yoghurt ni nzuri katika kulinda afya ya Mlaji ambao mtumiaji akitumia bidhaa hii Mara kwa mara inamsaidia mtu kujenga kinga imara katika mwili," amesema na kuongeza

"Uandaaji wa maziwa haya unaendana na vipimo maalum kwaajili ya kuhakikisha yanachemshwa kwa njia ya mvuke na kuongeza bacteria wazuri kwa ajili ya afya na baktreria hawa usaidia kuondoa bakteria wale ambao wanakuwa wabaya katika mwili," amesema

Amesema watanzania wajitahidi kunywa maziwa haya ili waweze kujenga miili yao na kuimarisha kinga za mwili.

No comments:

Post a Comment

Pages