July 22, 2020

Mc Pilipili aambulia kura moja jimbo la Bahi


NA MWANDISHI WETU

Msanii maarufu wa vichekesho nchini ambaye pia ni mshereheshaji, Emmanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili ameambulia kura moja kaika kura za maoni jimbo la Bahi lililopo mkoani Dodoma.

Katika jimbo hilo aliyeibuka mshindi ni Keneth Nolo aliyepata kura 259 akifuatiwa na Dornald Mejeti kura 210 pamoja na Omary Badueli aliyepata kura 32.

Mc Pilipili alichukua fomu ya kuwania Ubunge kwenye jimbo la Bahi Dodoma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mc Pilipili alichukua fomu ambapo alijinadi kwamba atawaondoa woga vijana na kuwahamamisha kushiriki katika masuala ya kuwania uongozi kwani Serikali ya awamu ya tano imekuwa na uwazi na ukweli.

"Nataka kuwatumika wana Bahi, nimejipima na kujitathimini kwamba naweza na ndio maana nikafanya maamuzi ya kuchukua fomu ya kukiomba chama changu kinipatie ridhaa ya kugombea nafasi ya Ubunge," alisema Mc Pilipili

Mc Pilipili ni mmoja wa wasanii wenye familia na amejaaliwa kupata mtoto mmoja na amekuwa gwiji wa sanaa za vichekesho na mshehereshaji.

No comments:

Post a Comment

Pages