July 22, 2020

RWEIKIZA AIBUKA KINARA KURA ZA MAONI KAGERA

 Makada wa CCM
 Wajumbe wakipoiga kura.
 
Na Lydia Lugakila, Bukoba
 
Mbunge wa Bukoba vijijini mkoani Kagera, Jasson Samson, Rweikiza amefanikiwa kutetea nafasi yake ya ubunge katika kura za maoni kwa kuibuka na ushindi wa kura 404.
Zoezi hilo la upigaji kura za maoni limefanyika katika uwanjwa wa Kaitaba uliopo manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.  
Akitangaza matokeo ya kura za maoni msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Nestory Kulinda mbele ya wajumbe hao amesema kuwa  jumla ya kura zilizopigwa ni 732 na  kura zilizoharibika ni kura 2 huku kura halali zikiwa ni 730 ambapo  Bwana Kyaruzi Edward amepata kura 26,  Engineer Ismail Nasoro kura 43, Kamgisha Yasin Matsawili kura 101 na Dokta Jasson Samson Rweikiza akiibuka na  kura 404.
Hata hivyo Jumla ya wagombea wa nafasi za ubunge katika kura za maoni jimbo la  Bukoba vijijini walikuwa ni 42 kati yao wanaume ni 41 mwanamke mmoja.

No comments:

Post a Comment

Pages