July 17, 2020

Mjumbe wa UWT autaka Ubunge Viti Maalum Morogoro

Na Janeth Jovin

MJUMBE wa Baraza Kuu UWT Taifa Dk. Lucy Mwanisawa, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama chake Cha mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro.



Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Dk. Mwanisawa amesema anaamini kuwa sasa ni wakati sahihi wa yeye kuingia bungeni na kutetea wanawake wenzake na k upinga mimba za utotoni.


"Kupitia nafasi yangu nitakayopewa nataka kumwinua mwanamke kiuchumi, kuwepo kwa kilimo bora na kupambania haki ya umiliki wa ardhi kwa akina mama," amesema

Mpaka sasa tayari wanachama zaidi ya 8000 wa CCM wameshachukua fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama kugombea ubunge katika majimbo mbalimbali.
Mjumbe wa Baraza Kuu UWT Taifa Dk. Lucy Mwanisawa akipokea fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama chake cha CCM kugombea Ubunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Pages