July 15, 2020

MKUU MPYA WA WILAYA YA MVOMERO ASHANGAZWA NA HATUA ZA MAENDELEO CHUO KIKUU MZUMBE

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero akiwa ameambatana na Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe wakati wa kutembelea mradi wa hosteli za wanafunzi Kampasi Kuu.
Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa hosteli za Wanafunzi kutoka Kampuni ya Suma JKT Injinia Issa Kanyaga akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa hosteli eneo la Maekani -Kampasi Kuu Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Albinus Mugonya (Mwenye kaunda suti nyeusi) akishauriana jambo na Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka (mwenye mwenye suti) kuhusu ujenzi ya hosteli Maekani Kampasi Kuu - Morogoro.
 
 
Morogoro, Tanzania
 
Mkuu Mpya ya Wilaya ya Mvomero Mhe. Albinus Mugonya, ametembelea Chuo Kikuu Mzumbe na kushangazwa na hatua kubwa za maendeleo katika ujenzi wa miundombinu.

Akiwa ameambatana na Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Bw. Abdallah Mdimu; walipokelewa na Menejimenti ya Chuo hicho ikiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof.
Lughano Kusiluka, ambaye amempongeza Mhe. Albinus kwa kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika maeneo yote ya vipaumbele vya Wilaya vinavyolenga kuwaletea wananchi maendeleo.

Ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kuteuliwa na Mhe. Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo; Mhe. Albinus amesema ameamua kwa dhati kufanya ziara yake ya kwanza kuwa katika Chuo hicho kwakuwa ana imani kubwa na Taasisi hiyo ya Elimu ya Juu nchini katika kutimiza ndoto na vipaumbele vyake kwenye kuwahudumia na kuwaletea wananchi maendeleo.

“Kwanza nimekuja kujitambulisha, pili kuomba ushirikiano na msaada katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mvomero kwani Chuo Kikuu Mzumbe kina watalaamu na
wabobevu katika nyanja tofauti; na tatu kutoa ushuhuda wa mchango wa wanataaluma katika kuleta maendeleo kwenye Halmashauri zetu endapo watashirikishwa kikamilifu na kuwa sehemu ya mikakati ya Halmashauri katika kufikia malengo” Alisisitiza
 
Miongoni mwa mambo aliyovutiwa chuoni hapo ni maendeleo katika ujenzi wa miundombinu yakiwemo mabweni ya wanafunzi yanayojengwa kwa ufadhili wa Serikali na jengo la ghorofa nne la vyumba vya madarasa na kumbi za mihadhara eneo la Maekani Kampasi Kuu – Morogoro linalojengwa kwa fedha za ndani. Mhe. Albinus Mugonya aliteuliwa 03 Julai 2020 na kuapishwa Ikulu Chamwino Dodoma tarehe 06 Julai, 2020 na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mkuu wa
Wilaya mpya waWilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Pages