July 15, 2020

TAKUKURU MKOANI PWANI YAOKOA MILIONI 35

 
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Pwani Suzan Rymond akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na utekelezaji wa majukumu ya  kazi zake ambazo wamezifanya kuanzia mwezi Aprili hadi juni mwaka 2020 pamoja na fedha ambazo wameweza kufanikiwa kuziokoa. (Picha na Victor Masangu).


VICTOR  MASANGU, PWANI

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rrushwa (TAKUKURU) imeokoa kiasi Cha Shilingi milion 35,000,000 kati ya milion 394,156335.30 ambazo ni fedha za malipo ya korosho kwa wakulima Mkoani Pwani.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Suzana Raymond alibainisha hayo jana wakati akitoa taarifa ya miezi mitatu ya Taasisi hiyo.

Alisema, Kampuni ya Mafubilo General Supplies ya jijini Dar es salam iliyonunua korosho za wakulima kwa mkopo kupitia Amcos za Visiga, Kongowe,Mwendapole,Mkombozi na Miembe saba zenye jumla ya Shilingi  milion 394,156,333.30.

Suzana alisema, malipo ya korosho hizo  yalisuasua  hadi pale TAKUKURU ilipoinhilia Kati na kufuatilia kuhakikisha mnunuzi analipa.

Mkuu huyo wa TAKUKURU alisema, mdaiwa amepewa maagizo ya kulipa mpaka amalize deni lote haraka iwezekanavyo ili wakulima wapate haki yao.

Katika hatua nyingine Taasisi hiyo imeokoa Shilingi milion 4,900,000 za Mwalimu mstaafu Yusuph Kimweri ambaye alikuwa amelipa kwa Ibrahim Masawe kupitia mkopo usiofuata kanuni taratibu na sheria zinazosimamiwa na Taasisi za fedha nchini kiasi Cha Shilingi 700,000 aliokopa mwaka 2018.

Akiongelea suala hilo Suzana alisema, kupitia riba deni lilikua na kufikia milion 13,000,000 ambalo Mstaafu alilipa mara baada ya kupokea pensheni yake ya kustaafu Mei 27 2020.

Mkuu huyo wa TAKUKURU alisema, baada ya kupokea malalamiko hayo walifanya uchunguzi wa kina na kubaini mtuhumiwa alifanya biashara ya kukopesha fedha kinyume na kanuni .

Imeelezwa kuwa baada ya mtuhumiwa kutambua kosa aliahidi kurejesha fedha hizo mpaka sasa amerejesha Shilingi milion 4,900,000 na atatakiwa kukamilisha kiasi kilichobaki Cha Shilingi milion 8,100,000.

No comments:

Post a Comment

Pages