July 16, 2020

MTIFUANO CCM UBUNGE, 700 WAJITOKEZA KUCHUKUA FOMU MKOANI SINGIDA

 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru (kushoto) akimkabidhi fomu mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Sara Mwambu.
 Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Jemima Richard Billiah (katikati) akionesha fomu yake baada ya kukabidhiwa juzi. Kushoto ni Mpambe wake Hamisi Soud na Kulia ni kaka yake, Pascal Billiah.
 Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Diana Chilolo, akionesha fomu yake baada ya kukabidhiwa juzi. Kulia ni Mpambe wake Jamila Juma. 
 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru (kushoto) akimkabidhi fomu Aysharose Mattembe aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, ambaye anatetea nafasi yake hiyo.
Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru (kushoto) akimkabidhi fomu aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Martha ambaye anatetea nafasi yake.
 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru (kushoto) akimkabidhi fomu mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Mhadhiri Dkt. Theresia Mnaranara.
  Mgombea Ubunge Singida Mjini, Charles Kisuke, akionesha fomu yake baada ya kukabidhiwa juzi.

  Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Noverty Kibaji (kulia) akimkabidhi fomu aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu ambaye anatetea nafasi yake.
   Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida Mjini, Hamis Shaban (kushoto) akimkabidhi fomu aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Musa Sima ambaye anatetea nafasi yake.
 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru (kushoto) akimkabidhi fomu mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Martha Gwau.

 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Noverty Kibaji (kulia) akimkabidhi fomu aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu ambaye anatetea nafasi yake.
 Mwanahabari Haris Kapiga (kulia) akikabidhiwa fomu kwa ajili ya kugombea Ubunge Jimbo la Iramba Mashariki.


  Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru (kushoto) akimkabidhi fomu mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Stellah Mwagowa.
 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru, akikabidhi fomu. 
 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Edina Kiguru, akikabidhi fomu.



Na Dotto Mwaibale, Singida


UCHAGUZI wa nafasi ya Ubunge mwaka huu umetia fora baada ya wagombea zaidi 700 kujitokeza kuomba ridhaa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika nafasi mbalimbali za majimbo na kata mkoani Singida.

Idadi hiyo imekuwa ni gumzo kwa wananchi na wana CCM ambapo kwa miaka iliyopita hakukuwa na wingi wa wagombea kama ilivyo uchaguzi wa mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana wakati akitoa taarifa za awali Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM  mkoani hapa, Ahmed Kaburu alisema kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu kunaonesha mwamko mkubwa na wanaikubali Serikali hii ya awamu ya tano jinsi inavyofanya kazi.


Akizungumzia mchakato wa uchukuaji wa fomu alisema kwa makundi yote manne ya vijana, wazazi, madiwani  viti maalumu  na majimboni wagombea 700 wamejitokeza kuchukua fomu kwa juzi tu hadi kufikia saa 10 jioni.

Alisema akianza na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi mpaka juzi jioni ni mgombea mmoja aliyekwisha chukua fomu kupitia wanawake ambapo kwa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM walikuwa wanne.

Kaburu alisema kwa Umoja wa Wanawake wa chama hicho UWT mpaka muda huo waliochukua fomu walikuwa 27 huko wagombea wote katika majimbo 8 ya Mkoa wa Singida wakiwa 119.

Aidha Kaburu alisema kwa nafasi ya udiwani waliichukua fomu katika kata zao walikuwa 420 huku madiwani wa viti maalumu ambao wanagombea kitarafa waliochukua fomu ni 129.

"Ndugu waandishi wa habari napenda kuwaambia kwamba tu kazi bado inaendelea na mwisho wa mchakato huu wa kuchukua fomu nitatoa majina ya wagombea wote na kata zote ili muwafahamu" alisema Kaburu.

No comments:

Post a Comment

Pages