July 16, 2020

Mwenye Mapacha wanne achukua fomu ya kuwania ubunge viti maalum UWT Kinondoni

Na Makuburi Ally

MWANADADA Radhia Japhet Solomon mwenye mapacha wanne amejitosa katika kinyang'anyiro cha kuwania ubunge viti maalum Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Radhia ni mmoja wa wagombea zaidi ya 180 waliojitokeza katika mchakato huo tangu Julai 14.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Haule Wanawake wameonesha kwamba wanaweza kutekeleza majukumu ya jamii kwa sababu hawajawahi kushindwa katika nafasi wanazopewa.

Haule alisema kujitokeza kwa idadi kubwa ya wagombea zaidi kumetokana na hamasa waliyoifanya kuanzia ngazi ya matawi Kata Wilaya Mkoa na Taifa.

Naye Radhia alisema amejitokeza kuchukua fomu baada ya kujipima na kujiona kwamba anatosha kuitumikia nafasi hiyo.
 Radhia Japhet Solomon mwenye mapacha wanne akipokea fomu ya kuwania ubunge viti maalum Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Radhia Japhet Solomon mwenye mapacha wanne, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu ya kuwania ubunge viti maalum Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Radhia Japhet Solomon mwenye akiwa na mapacha wake.

No comments:

Post a Comment

Pages