July 08, 2020

PROFESA MANYA AFANYA ZIARA KWENYE BANDA LA UDSM

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya, akisaini kitabu cha wageni.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya, akizungumza akipata maelezo kwenye banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Maonesho ya Sabasasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 07 Julai, 2020.


Na Mwandishi Wetu

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya amefanya ziara kwenye Banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa wataalam mbalimbali, Profesa Manya amempongeza Makamu Mkuu wa Chuo hicho pamoja na Idara zote kwa kazi nzuri kwa kuwa wabunifu kwenye uendelezaji wa taaluma mbalimbali.

" Tukiwa kwenye uchumi wa kati hatuna budi kuhakikisha tunaongeza ubunifu kwenye utoaji taaluma ili kuendana na kasi ya uchumi wa viwanda, " amesema Profesa Manya.

Katika hatua nyingine  akizungumza kupitia mahojiano maalum na waandishi wa habari kwenye banda la Tume ya Madini Profesa Manya amewataka wafanyabiashara wa madini kuendelea kutumia masoko ya madini yaliyoanzishwa.

Akielezea mwenendo wa masoko nchini, Profesa Manya amesema kuwa masoko ya madini yameendelea kufanya kazi hususan kwenye dhahabu licha ya kuwepo kwa changamoto ya ugonjwa wa korona katika miezi kadhaa iliyopita.

Ameongeza kuwa,  katika kuhakikisha madini ya tanzanite yanatambulika kimataifa kama zao la Tanzania na kukuza utalii, Serikali iliamua kununua madini ya tanzanite yaliyogunduliwa hivi karibuni na Saniniu Laizer huko Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara kwa bei ya soko la dunia.

No comments:

Post a Comment

Pages