July 08, 2020

BANDA LA TTCL LAVUTIA WENGI MAONESHO YA SABASABA

Baadhi ya wateja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakipata huduma mbalimbali walipotembelea Banda la TTCL leo katika Maoneshoya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Leonard Laibu (kushoto) akimuonesha mmoja wa wateja moja ya bidhaa za simu za kisasa za TTCL ndani ya Banda la TTCL leo kwenye Maoneshoya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wa TTCL (kulia) wakipata huduma mbalimbali walipotembelea Banda la TTCL leo katika Maoneshoya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wateja wa TTCL (kushoto) pamoja na wananchi wengine wakipata huduma mbalimbali walipotembelea Banda la TTCL leo katika Maoneshoya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni mmoja wa wafanyakazi wa TTCL akihudumia wateja ndani ya banda la TTCL katika leo kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni mmoja wa wafanyakazi wa TTCL akihudumia wateja ndani ya banda la TTCL katika leo kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

BANDA la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo siku ya Sabasaba limekuwa kivutio kikubwa kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Ikiwa leo ni Siku Kuu ya Sabasaba maarufu kwa maonesho hayo, idadi kubwa ya watu wamefurika kujionea bidhaa na huduma mbalimbali za kuvutia ambazo zinaoneshwa katika maonesho hayo, ikitofautisha na siku ya jana.

Akizungumza katika banda la TTCL, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa shirika hilo, Bw. Leonard Laibu alisema idadi kubwa ya wananchi wamepita kujionea bidhaa na huduma tunazozitoa kwenye maonesho hayo.

Bw. Laibu alisema licha ya kuonesha bidhaa mbalimbali za kisasa zinazotolewa na kampuni hiyo, kwa kuwajali wateja wao wanatoa huduma zote muhimu kwa wateja katika maonesho hayo.

"...Siku zote TTCL tunawajali na kuthamini wateja wetu, hivyo mteja akifika ndani ya banda hilo  anapata huduma zote muhimu..., ndiyo maana hata sasa unaona idadi kubwa ya wateja na wananchi wanapita humu, kuangalia na pia kujipatia huduma wanazohitaji," alisema meneja huyo, kitengo cha Huduma kwa Wateja.

Akifafanua zaidi alisema idadi kubwa ya wateja wanahudumiwa huduma za usajili wa laini, kurudisha laini zilizopotea au kuharibika, vifaa vya intaneti kama modem na simu za kisasa za TTCL, huduma za T-PESA, huduma za mkongo wa taifa wa mawasiliano na huduma za Data Senta.

Hata hivyo, aliwaomba wananchi wanaofika kutembelea Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea kupita ndani ya banda la TTCL kujionea mambo mazuri yalioandaliwa kwa wateja na wananchi wanaopita kujionea.

Alibainisha bado TTCL inawakumbusha wananchi hasa wapenzi wa filamu nchini kufurahia ofa ya huduma ya 'T-Burudani' toka TTCL kwa shilingi 2000 tu na kumwezesha mteja kuangalia filamu na tamthilia aipendayo bila ya kuwa na mtandao wa intaneti.

“Huduma ya T-Burudani ya TTCL ni rahisi inamuwezesha mteja kupakua filamu bila kutumia kifurushi cha intaneti, mteja ataweza kuangalia filamu zote za ndani ya nchi pamoja na kimataifa, mteja ataweza kupakua kupitia simu janja ya mkononi pamoja na kompyuta ya kiganjani ‘Tablet’,” alisema Bi. Nzalayaimisi.
Wananchi na wateja ndani ya banda la TTCL leo kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages