July 21, 2020

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika Oktoba 28, mwaka huu

Na Janeth Jovin

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imesema kuwa Uchaguzi Mkuu wa Udiwani, Ubunge na Urais utafanyika Jumatano ya Oktoba 28, 2020.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Kaijage amesema uteuzi wa wagombea utakuwa Agosti 25, 2020 na kampeni zitaanza rasmi Agosti 26 na kumalizika Oktoba 27, mwaka huu.

“Siku ya uchaguzi itakuwa tarehe Oktoba 28, mwaka huu,” amesema Kaijage

Hii itakuwa mara ya kwanza Uchaguzi Mkuu unafanyika katikati ya wiki yaani Jumatano tofauti na chaguzi zilizopita ambazo zilikuwa zikifanyika Jumapili

No comments:

Post a Comment

Pages