July 07, 2020

Vodacom yatoa punguzo la bei ya simu janja za Smart Kitochi kwenye maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya sabasaba

Meneja wa maduka ya Rejareja Vodacom Tanzania PlC, Vanessa Mlawi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea banda la Vodacom kwenye maonesho ya 44  ya biashara ya kimataifa ya sabasaba kuhusu punguzo la bei kwa simu za Smart Kitochi zinazopatikana kwa shilingi 45,000/- na bidhaa mbalimbali zinazopatikana bandani hapo leo.
 Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (wa pili kushoto) pamoja na Msaidizi wa Mipango Vodacom Tanzania Foundation, Kelvin Boya wakiwaelezea wateja kuhusu huduma ya Instant School  walipotembelea banda la Vodacom kwenye maonesho ya 44  ya biashara ya kimataifa ya sabasaba leo.
 Mtoa huduma kwa wateja Vodacom, Oliver Nyasa (kulia) akimsikiliza mteja aliyetembelea banda la Vodacom kwenye maonesho ya 44  ya biashara ya kimataifa ya sabasaba leo.
 Mtoa huduma kwa wateja Vodacom, Faraja Mwaseke (kulia) akiwasikiliza wateja waliotembelea banda la Vodacom kwenye maonesho ya 44  ya biashara ya kimataifa ya sabasaba leo.

No comments:

Post a Comment

Pages