July 07, 2020

WAFUGAJI KINONDONI WAOMBA KUKOPESHWA MASHINE

Mwenyekiti wa Ushirika wa wafugaji wa ng'ombe Wilaya ya Kinondoni,Kajia Mrita akionyesha moja za mashine za usindikaji wa maziwa zilizopo katika banda la uvuvi na Mifugo katika maonesho ya 44 ya kimataifa ya  Biashara  sabasaba.


Na Tatu Mohamed
WAFUGAJI wa Ng’ombe wa maziwa Wilaya ya Kinondoni, Wameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi nchini pamoja na Bodi ya Maziwa kuwasaidia kuwakopesha mashine za usindikaji maziwa.

Ombi hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa Ushirika wa Wafugaji hao, Kajia Mrita alipokuwa akizungumza katika viwanja vya maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba'.

Alisema hali ya uzalishaji wa maziwa katika wilaya yao ipo juu ukilinganisha na miaka ya nyuma hivyo watakaposaidiwa mashine hizo, itawaongezea thamani katika usindikaji wa maziwa.

“Tutakapo saidiwa mashine hizi na serikali tunaamini kwa kiasi kikubwa tutakapo yasindika maziwa haya, kuongea thamani yatakuwa na bei nzuri zaidi kuliko vile tunapokamua na kuuza moja kwa moja,” amesema.

Ameongeza kuwa mashine hizo zilizopo katika maonesho hayo zenye ujazo wa lita 200 hadi 500 endapo watazipata wanaamini soko la maziwa litazidi kuongezeka.

No comments:

Post a Comment

Pages