July 07, 2020

NAIBU WAZIRI DK. NDUMBARO NA JAJI WA MAHAKAMA KUU WATEMBELEA BANDA LA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

 Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Seif Kulita akipokea zawadi aliyopewa na Ofisa wa Shirika la Posta Aneth Mdamu (Kulia) ndani ya jengo la Posta kwenye viwanja vya maonesho ya sabasaba.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfriKa Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro, akifuatilia maelezo kwa vitendo jinsi ya kujiunga huduma ya Posta Kiganjani huku akiwa amezungukwa na baadhi ya maofisa waandamizi wa Shirika la Posta Tanzania.


Na Janeth Jovin

NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfriKa Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam,  Seif Kulita wametembelea banda la Shirika la Posta Tanzania lililopo ndani ya viwanja vya maonesho 44 ya kimataifa ya biashara (Sabasaba).

Dk. Ndumbaro  na Jaji Kulota walitembekea banda huyo juzi na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Posta kwenye maonesho hayo.

Pamoja na kutembelea banda la Posta Dk. Ndumbaro alijisajili na mfumo wa Posta Kiganjani ambao utamuwezesha kumiliki sanduku la barua kupitia simu yake ya mkononi.

Akizungumza mara baada ya kujisajili, Dk. Ndumbaro alipongeza mabadiliko makubwa ya utoaji huduma za Posta aliyoyaona ndani ya banda hilo na kukumbushia huduma ya Telegraphic Money Order ambayo alikua akiitumia kupitia Shirika la Posta kipindi cha nyuma.

 Naye Jaji Kulita alipata fursa ya kuona na kupata maelezo ya kina juu ya umuhimu wa huduma ya posta kiganjani mwako ambapo alipongeza mabadiriko hayo.

Huduma hiyo mpya ya Posta Kiganjani
 itamuwezesha kila mtanzania kumiliki sanduku la barua kupitia simu yake ya mkononi.

Kupitia huduma hiyo, watanzania
awatahitajiki tena kuwa na boski la barua na kwenda nalo katika ofisi za Posta kupata huduma bali atatakiwa kutumia simu yake ya mkononi ambayo ndio itakuwa sanduku lake la barua.

Maonesho ya biashara ya Sabasaba yalianza rasmi tarehe 1 julai 2020, na yatamalizika tarehe 13 Julai 2020 huku Shirika la Posta likiendelea kuwasisitiza watanzania wote kutembelea banda la Posta ndani ya maonesho hayo.

No comments:

Post a Comment

Pages