HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 24, 2020

ROSE MUHANDO KUNOGESHA TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2020

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu maandalizi ya Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania litakalofanyika Septemba 6, 2020 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwimbaji wa nyimbo za injili, Rose Muhando.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari.
 Mwimbaji wa nyimbo za injili, Rose Muhando, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, leo Agosti 24m kuhusu ushiriki wake katika tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2020.
 

DAR ES SALAAM, TANZANIA

Mwimbaji wa nyimbo za injili, Rose Muhando, amewataka watu kujitokeza kwa wingi katika tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu litakalofanyika Septemba 6, 2020 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mwimbaji huyo alisema kuwa "Nimejipanga vizuri pamoja na waimbaji wengine nawahakikishia wale wote watakaofika katika tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2020 watapata burudani ya uhakika".

"Hatujawai kupoa na hatupoi uwanja wa Uhuru tutawasha moto katika kuombea uchaguzi wa mwaka huu, kwa kuwa Mungu wetu hajawai kupoa hivyo tunatarajia kuwasha moto husiozimika na tumejipanga vizuri, watanzania mjitokeze kwa wingi bila kukosa kushuhudia uhondo huo"alisema Rose Muhando.
 
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama, ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo alisema kuwa tamasha hilo lilipaswa kufanyika Agosti 23 lakini lilisogezwa mbele hadi Septemba 6 kutokana na shughuli za michezo katika Uwa ma wa Uhuru.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na waimbaji watakaotumbuiza wanaendelea kujifua ili kukata kiu ya watakaohudhuria, nasi kama waratibu wa tamasha, tumeongeza idadi ya wasanii watakaotumbuiza siku hiyo ya kuombea Uchaguzi Mkuu,” amesema.

Ukiachana na Bonny Mwaitege, Christopher Mhangira, Christina Shusho na Rose Mhando aliowataja siku ya utambulisho wa tamasha hilo lisilo la kiingilio, Msama amewaongeza Martha Mwaipaja, Upendo Nkone, Faustine Munishi na Mercy Changula.

“Huyu Faustine Munishi anayetambulika na wengi kwa wimbo wa Malebo, atakuja tamashani na Malebo mwenyewe ili watu wamuone huyo aliyemuimba katika wimbo wake huo,” alisisitiza Msama huku akisema usalama utakuwa mkubwa.

Kuhusu usalama wa watu watakaohudhuria, mali zao na familia zao kwa ujumla, Msama alisema: “Kutakuwa na usalama wa hali ya juu kutoka kwa askari wa Jeshi la Polisi na askari wa kampuni binafsi ili kuhakikisha kila anayeingia anakuwa salama.”

“Tunawaalika watu wa madhehebu na dini nyingine waje, hili ni tamasha la Watanzania. Waje ili kwa pamoja tuliombee taifa letu, tuuombee Uchaguzi Mkuu uende kwa salama na amani,” alisema Msama anayeratibu pia Matamasha ya Pasaka na Krismasi.

Akimuelezea Rose Mhando, Msama alifichua kuwa nyota huyo amejipanga kwa maandalizi makali, kutumbuiza nyimbo za Injili za zamani na mpya na kwamba kama ratiba zitaruhusu.

No comments:

Post a Comment

Pages