August 22, 2020

UCHACHE WA VIWANDA VYA MBOLEA YASABABISHA BEI KUWA JUU

 

 Na Asha Mwakyonde
 

KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amesema kuwa uchache wa viwanda vinavyozalicha mbolea ya Urea unasababisha wakulima mkoani Kagera kuuziwa mfuko wa mbolea hiyo kilo 50 kwa shilingi elfu 80 hadi
90.


Haya aliyasema jijini Dar es Salaam jana katika ziara yake ya siku nne  iliyoanzia jijini hapa yenye lengo la kutembelea Viwanda vinavyozalisha mbolea hapa nchini  na kuona kiwango kinachozalishwa na viwanda vya ndani na uwezo wake wa kuzalisha, alisema alipokea malalamiko kutoka kwa wakulima wa Kagera.


Katibu huyo alisema baada ya malalamiko hayo alikagundua kuwa tatizo linalosababisha mbolea iuzwe kwa bei ghali ni kutokana na uchache wa viwanda ambavyo vinazalisha kwa kiwango kidogo ambacho hakitoshelezi mahitaji ya wakulima.
 

Alisema ameamua kufanya ziara hiyo ili ajue jinsi gani wanaweza kuwasaidia wenye viwanda ili wazalisha mbolea kwa wingi iwatosheleze wakulima.


"Mfano nilikuwa mkoani Kagera Mfuko wa kilo 50 wa mbolea ya Urea mkulima anaununua kwa shilingi elfu 80 hadi 90, nikagundua kuwa tatizo linalosababisha mbolea iuzwe kwa bei ghali ni kutokana na uchache wa viwanda ambavyo vinazalisha kwa kiwango kidogo ambacho hakitoshelezi mahitaji ya wakulima,"alisema Katibu Kusaya.


Katibu huyo alisema  takwimu zinaonyesha kuwa hapa nchini kuna viwanda 12 tu vinavyozalisha mbolea ambapo Minjingu ndio kiwanda pekee kikubwa kinachozalisha mbolea ambayo yapo chini ya mahitaji ya wakulima hapanchini.
 

Katika ziara hiyo aliofanya katika kiwanda cha Guavay Company limited kinachozalisha mbolea ya Organiki ya Hakika Katibu amesema mahitaji ya mbolea kwa Tanzania ni zaidi ya laki sita na nusu hivyo viwanda vilivyopo vikizalisha mbolea ni tani elfu 38 tu.


"Upungufu huu wa mbolea unasababisha uagizwaji wa mbolea nyingi toka nje ya nchi hivyo kuwepo kwa changamoto kubwa ya uagizaji wa mbole toka nje ya nchi,"alisema.
 

Hata hivyo amesema serikali imeweka mikakati ya kuwashawishi wawekezaji kuwekeza katika viwanda vya mbole ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mbolea hapa nchini na kupunguza changamoto ya bei kwa wakulima ili wazalishe kwa wingi.


Kwa upande wake Dkt Stephano Ngailo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRAC) amesema uzalishaji bado ni mdogo ukilinganisha na uhitaji ambapo kwa sasa uzalishaji ni asilimia 6 na mbolea toka nje ni asilimia 94.
 

Alisema jitihada kubwa inafanywa na Serikali kuhakikisha kuwa
uwekezaji mkubwa unafanyika katika viwanda vya mbolea ili kupunguza gharama za uwekezaji kwa mkulima ambapo lengo la mamlaka ya mbolea ni kuhakikisha kuwa kuna upatikanaji wa mbolea bora kwa mkulima na kwa bei nafuu.
 

Naye Latifa Mafumbi mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Guavay Company limited alisema changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na udogo wa eneo la kuzalisha ambapo soko la mbolea za organiki linakuwa ambapo kwa mwaka wanazalisha tani elfu mbili huku uhitaji ukiwa ni tani elfu 20.


Hata hivyo aliiomba Serikali kuwasaidia kutoa uelewa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa mbolea za Organiki kwani muamko wao ni mdogo sana ukizingatia mbolea hizo zinasaidia kurutubisha udongo kwani tafiti zinaonyesha kuwa udongo wa Tanzania rutuba yake inashuka.
 

Ziara hiyo itahusisha mikoa minne ambayo ni Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro Arusha na Manyara.

No comments:

Post a Comment

Pages