Katibu Mkuu wa Tanzania Refugee and Migration Network (TAREMINET), ABEID Kasaizi akielezea warsha ya siku moja ya wadau wa msaada wa kibinadamu iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri Mwandamizi wa Shule Kuu ya Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), Prof. Khoti Kamanga akifafanua jambo kuhusu dhana ya
ushirikiano katika mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs). NA SULEIMAN MSUYA
MASHIRIKA
yasiyo ya Kiserikali nchini Tanzania (NGOs) yanayojihusisha na kutoa
msaada wa kibinadamu yameshauriwa kushirikiana ili yaweze kufikia
malengo waliyojiwekea.
Ushauri
huo umetolewa na Mkurugenzi wa Program wa International Councils of
Volunteers Agency (ICVA), Michael Hyden wakati akitoa mada kwenye warsha
ya siku moja kuhusu dhana nzima ya ushirikiano kwa wadau wa masuala ya
msaada wa kibinadamu jijini Dar es Salaam.
Warsha
hiyo iliandaliwa na Mtandao wa Mashirika yanayoshughulika na kutoa
msaada wa kibinadamu la Tanzania Refugee and Migration Network
(TAREMINET).
Hyden
alisema popote kwenye mafanikio msingi mkubwa ni ushirikiano wa wadau
husika na kwamba dhana ya kila mtu kujipendelea itakuwa changamoto.
Mkurugenzi
huyo alisema umoja na ushirikiano utaweza kuishawishi Serikali,
Mashirika yaliyopo chini ya Umoja wa Mataifa (UN) na mengine mengi
kuwasaidia kutimiza malengo ya msaada wa kibinadamu.
"Niwe
muwazi kuwa iwapo mnataka kufanikisha malengo yenu mnatakiwa kuwa
pamoja ili muimbe pamoja jambo ambalo litawarahisishia kufikia wadau
wote katika muhimu na sisi tutasaidia ambapo mnakwama kama ni masuala ya
kisheria iwapo kuna changamoto hiyo," alisema.
Alisema nchi ambazo NGOs zinafanya kazi pamoja mafanikio ni mengi tofauti na zile ambazo zinafanya kila mtu mwenyewe.
Alisema
ICVA wanapromoti kanuni za msaada wa kibinadamu ziweze kutekelezwa
katika nchi husika kwa kuwa wamesaini mikataba mbalimbali ya Kimataifa.
Mkurugenzi
huyo alisema ushirikiano huo utafanikishwa na uongozi bora, usimamizi,
uratubu, ushirikishwaji, uwazi na mengine muhimu kwenye taasisi.
Mwenyekiti
wa TAREMINET, Janemary Ruhundwa warsha hiyo imejikita kujadili dhana
nzima ya ushirikiano katika ngazi ya NGOs za ndani ya nchi katika utoaji
wa msaada wa kibinadamu nchini.
Alisema
kumekuwepo na mjadala mpana duniani tangu mwaka 1990 ila dhana hiyo
haijatekelezwa kisawasawa na kuonekana kwa jamii husika.
"Warsha
hii itatupa muongozo wa nini kifanyike hapa nchini kutekeleza dhana ya
ushirikiano katika eneo la msadaa wa kibinadamu kwani makubaliano
yalifikiwa bado tupo nyuma kiutekelezaji," alisema.
Ruhundwa
alisema bado NGOs nyingi zinaamini katika kusubiri mashirika ya
kimataifa kusambaza dhana hiyo jambo ambalo linawachelewesha.
Katibu Mkuu wa TAREMINET, Abeid Kasaizi alisema mtandao huo ni muunganiko wa mashirika 12 ya msaada wa kibinadamu Tanzania.
Alisema
warsha ya leo imelenga kuona ni namna gani wanaweza kutumia nguvu ya
pamoja katika kutatua majanga yanayopata nchi kwa pamija.
"Kuna
majanga kama mafuriko, tetemeko na mengine ambayo yanahitaji NGOs
zinazojihusisha na msaada wa kibinadamu kutoa msaada bila kubaguana.
"
Sisi tumeamua kupigania msaada wa kibinadamu kwa miaka mingi hivyo
tunapswa kuwa pamoja kupitia jukwaa la TAREMINET ili tusisambaze
rasilimali zinazopatikana na wahanga watapata kilichobora
zaidi,"alisema.
Kwa
upande wake Mhadhiri Mwandamizi wa Shule Kuu ya Sheria na Kituo cha
Wakimbizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Khoti Kamanga
alisema tatizo la wakimbizi ni kubwa duniani na njia sahihi ya
kukabiliana nayo ni wadau wote kushirikishwa.
Prof.Kamanga
alisema dhana ya ushirikiano inataka kuwe na lugha moja shirikishi na
sio watu fulani kufanya maamuzi kwa niaba ya kundi fulani.
Alitolea
mfano janga la wakimbizi pamoja na kwamba asilimia 83 wanatoka nchi
maskini lakini sera kuhusu kundi hilo zinatungwa na nchi tajiri jambo
ambalo sio sahihi.
"Pia
mgawanyo wa fedha unafanyika huko katika nchi tajiri jambo ambalo
halileti dhana ya ushirikiano inakosekana kwa nchi maskini ambazo ndizo
zenye tatizo," alisema.
Mhadhiri
huyo alisema changamoto nyingine ambayo inaonekana kutokana na
kukosekana kwa ushirikiano ni nchi maskini kushindwa kufanya utafiti wa
kina wa hali halisi ya tatizo.
Alisema
ni wakati muafaka kwa mashirika ya kimataifa na wadau wa maendeleo
kuwezesha wataalam ili wafanye utafiti wa hali halisi ya wakimbizi
nchini na wahitaji wa msaada wa kibinadamu.
No comments:
Post a Comment