September 10, 2020

Benki ya CRDB yapewa dhamana ya bil.110/- kuboresha miundombinu

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
 
 
Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imepokea dhamana ya Sh. Bilioni 110 kutoka kwa Kampuni ya GuarantCo ambayo ni dhamana ya maika mitano kwa ajili ya maboresho ya utendaji hasa kwenye miundombinu ya sekta mbalimbali kiuchumi.


GuarantCo ni Kampuni ya Maendeleo ya Miundombinu (PIDG) yenye maskani yake Nchini Uingereza.

Akizungumza na wanahabari kuhusu dhamana hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema dhamana hiyo itaongeza uwezo wa benki ya CRDB kuwekeza kwenye miradi ya kimkakati na mipango ambayo inalinufaisha taifa ambayo inalinufaisha taifa na watanzania wote.
 
Alisema lengo la dhamana hiyo ni kujenga mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa kushirikiana ili kuchichimua ukuaji wa uchumi hususani kwenye uwekezaji mkubwa wa miundombinu na nishati.

Nsekela alisema ushirikiano wa Benki ya CRDB na GuarantCo utasaidia mipango ya serikali katika kufadhili miradi mikubwa ya miundombinu kwa kupanua mitaji na mikopo ya gharama nafuu kwa wakandarasi.

“Mbali na kuongeza upatikanaji wa fedha kwa wafanyabiashara, miradi inayofadhiliwa chini ya makubaliano ya GuarantCo itakuwa katika sarafu ya ndani, inayoepuka hatari ya kupoteza fedha za kigeni.

"Ushirikiano wetu unaonesha utayari yetu kwenye kujitolea kwetu katika kusaidia ukuaji wa uchumi wa nchi…"tunafurahi tunashirikiana kimkakati kuchunguza miundombinu ya ubunifu wa kifedha na kufadhili miradi ya miundombinu hapa nchini,” alisema Nsekela.

No comments:

Post a Comment

Pages