Mtoto wa darasa la saba, Veronica Anthony (17) ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na baba yake mzazi Anthony Costantine (50) baada ya kudai kuwa amechelewa kurudi nyumbani.
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mwandamizi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro, amesema tukio hilo limetokea saa mbili usiku maeneo ya Kayenze kata ya Kayenze wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Kamanda Muliro amesema mtoto huyo aliuawa kwa Kupigwa na Kitu Kizito Kichwani na Baba yake Mzazi Costantine baada ya Kile kinachodaiwa kurudi nyumbani Kwao akiwa amechelewa majira ya usiku kitendo kinachodaiwa kumkasirisha baba yake mzazi na kuamua Kutoa adhabu ya Kikatili kwa binti yake Iliyosababisha mauaji.
Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa uchunguzi wa daktari na kuongeza kuwa mtuhumiwa ambaye ni Baba mzazi wa marehemu amekamatwa na atafikishwa Mahakamani kwa hatua za Kisheria.
Kamanda Muliro amesema katika tukio jingine, Septemba 9, mwaka huu majira ya saa moja usiku huko maeneo ya Mhonze “a”, Kata ya Shibula, Wilaya Ya Ilemela, Mkoa Wa Mwanza, Emmanuel Joseph (49), Msukuma, Mkulima na Mkazi Wa Kijiji Cha Mhonze ‘a”, aliuawa baada Ya kupigwa na kitu Kizito Utosini na ndugu yake Mussa Majuto, Miaka 35, Msukuma, Mkulima Na Mkazi Wa Mhonze
Amesema kiwa inadaiwa marehemu alikua akimtuhumu mtuhumiwa kumwibia Simu Yake aina ya Tecno ya Batani yenye thamani ya Tsh 40,000/=. Mwili Wa Marehemu umehifadhiwa Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa Ya Sekou Toure Kwa uchunguzi wa Daktari. Aidha Mtuhumiwa amekamatwa Upelelezi unakamiliswa na atafikishwa Mahakani Haraka Iwezekanavyo
Hata hivyo amesema Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza linatoa wito kwa wazazi, walezi na familia Kwa Ujumla kuwa makini na adhabu wanazotoa kwa watoto kwani zinaweza kuwapelekea Kutenda Ukatili dhidi ya Watoto na kuleta madhara makubwa katika familia na baadae kufikishwa Mahakamani Kwa makosa ya Jinai.
"Pia Polisi Itaendelea kuwachukulia hatua kali Za Kisheria Watu Wote Wasioheshimu Sheria Za Nchi na Kutaka kuvuruga zoezi zima la Uchaguzi Mkuu kwa aina yoyote," amesema Muliro .
No comments:
Post a Comment