Mbombea udiwani kwa tiketi ya CCM katika Kata ya Makurumla, Dar es Salaam, Bakari Kimwanga akiwaomba kura wananchi aliponadi sera za CCM
katika Mkutano wa ufunguzi wa Kampeni za CCM, juzi katika Kata hiyo.
NA ASHA MWAKYONDE
MGOMBE udiwani Kata ya Makurumla kwa tiketi ya Chama cha
Mapinduzi (CCM), Bakari Kimwanga ametaja vipaumble vyake endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi kuiongoza kata hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kampeni zake
zilizofanyika katika viwanja vya Kwa Jongo Mburahati mgombea huyo alisema akipata ridhaa ya wananchi atahakikisha chanagamoto za kijamii zinazowakabili wananchi wa kata hiyo zinapungua kwa kipindi cha muda mfupi.
Mgombea huyo alisema kata hiyo ina changamoto nyingi ambazo zinahitaji watu makini kuzitatua na lengo la chama hicho ni kuleta ufumbuzi wa muda mfupi kutatua changamoto hizo.
Alivitaja vipaumbele vyake kuwa ni elimu, afya, miundombinu, mikopo kwa akina mama, vijana na kwa watu wenye ulemavu.
Mgombea huyo alisema kwa upande wa sekta ya elimu miundombinu yake bado hairidhishi hasa katika shule ya msingi Mianzini baadhi ya madarasha ni hatarishi kwa afya za watoto.
Alisema kituo cha Afya cha Mianzini bado kuna masononeko ya wananchi kutotoa huduma bora na kwamba endapo atachaguliwa atahakikisha vifaa tiba vinapatikana kwa wakati pamoja na madakrari. Kimwanga alieleza kuwa wakiangalia suala la uwekezaji wa mikopo inayotolewa inaangalia undugu hivyo endapo watapata ridhaa wataenda kusimamia asilimia 10 ya mikopo inayotolewa na Halmashauri.
"Tutasimamia mikopo hii iende kwa makundi ya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu bila kuangalia undugu kama inavyotolewa kwa sasa tutatoa kwa wote na kila mtu afye na chake,"alisema.
Alisema kwa upande wa miundombinu watajenga kingo za mifereji inayosababisha mafuriko kwa baadhi ya maeneo na kwamba barabara zilizopo haziendani na hadhi ya watu wanaoishi katika kata hiyo.
Mgombea hiyo alieleza kuwa kukosekana kwa uongozi thabiti ni
kukosekana kwa uwajibikaji kwa watu waliopewa ridhaa hivyo wanahitaji kuleta utabuzi ndani ya muda mfupi.
"Wananchi chagueni CCM mafiga matutu ili tuweze kuongea lugha moja ya maendeleo ya kata hii kupitia Rais, mbunge na diwani kero zenu nitazifikisha kwa kaka yangu Profesa Kitila Mkumbo ambaye atakuwa bungeni ili aweze kunisaidia," alisema.
Aliongeza kuwa wanaposema suala la kusukuma mbele maendeleo linahitaji watu makini ili kuweza kutatua changamoto hizo hivyo wananchi hao wakiwachagua madiwani wote wa chama hicho katika jimbo la Ubungo kutakuwa namaendeleo makubwa.
"Mkituchangua madiwani wote takaingia Halmashauri hakika maendeleo mtayaona maana tutafanikiwa kuwa na Meya anayetoka CCM hivyo fedha zote za miradi tutakuwa nazo, " alisema mgombea huyo.
CAPT
Mbombea Udiwani kwa tiketi ya CCM katika Kata ya Makurumula, Dar es Salaam, Bakari Kimwanga akiwaomba kura wananchi aliponadi sera za CCM katika Mkutano wa ufunguzi wa Kampeni za CCM, jana katika Kata hiyo
No comments:
Post a Comment