Na Ghisa Abby,Lindi
Afisa
toka Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) Shaban Mafita
ameeleza kuwa asilimia 80 ya uharibifu wa misitu nchini hufanyika
katika ardhi za vijiji na shughuli kubwa inayofanya uharibifu huo ni
kilimo cha kuhama hama ambapo hekta 17.6 milioni za misitu zilizopo
kwenye ardhi hizo za vijiji bado hazijarasimishwa kisheria.
Aidha
afisa huyo amesema hekta 1.4 milioni pekee ndizo zilizorasimishwa huku
hekta 3 milioni kati ya hekta hizo 17.6 zipo kwenye halmashauri za
serikali za mitaa.
Ameeleza
hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuutambulisha
mradi wa Haki katika Misitu awamu ya pili wenye lengo la kampeni ya
misitu kwa kila kijiji na hiyo ni baada ya kuona kuwepo kwa changamoto
zinazotokea kwenye usimamizi shirikishi wa misitu ambayo inasimamiwa
TFCG pamoja na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania
(MJUMITA).
Mafita amesema
wakati Tanzania ikiwa na hekta 48.1 milioni sawa na asilimia 54.4 ya
maeneo Tanzania bara, misitu inayohifadhiwa katika ardhi za vijiji ni
hekta 22 milioni.
“Shughuli
za uanzishwaji wa mashamba kupitia kilimo cha kuhama ndizo zimekuwa
zikifanya uharibifu wa mazingira na hii ni takwimu kwa mujibu wa ripoti
ya Nafoma na kwa kiasi kikubwa zinaonyesha kuwa hekta 460,000
zinaharibiwa kila mwaka na kwa kiasi kikubwa eneo hilo linatokana na
kutorasimishwa hasa maeneo ya vijiji,”amesema Mafita.
Amesema
Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine katika masuala ya Misitu
lazima itoe kipaumbele kwenye misitu ambayo haijarasimishwa ili iweze
kurasimishwa na vijiji vinavyofanya usimamizi shirikishi ya misitu kwa
pamoja isimamiee kwani imekuwa na manufaa kwa jamii kwa kupata mapato
kupitia usimamizi na uvunaji endelevu ambao unafanyika kupitia utatibu
wa uvunaji wanaouanzisha katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na fedha
wanazozipata kufanyia shughuli za maendeleo kama ujenzi wa
shule,madarasa na kupata bina za afya.
“Faida
hizi za misitu tunataka kupeleka mbali kuona kwamba ile misitu ya hekta
17.6 milioni na yenyewe inasimamiwa katika utaratibu ili kunusuru
misitu kuendelea kuharibiwa katika namna ambayo inaonekana kama uchomaji
wa mkaa, uvunaji mbao na ukataji miti kiholela,”amesema.
Mafita
amesema kampeni hiyo isiishie kwa viongozi wa kiserikali lakini
viongozi wa kisiasa wana nafasi kubwa ya kuhakikisha mafanikio ya
usimamizi shirikishi wa misitu yanaingizwa katika Ilani na program za
serikali ambazo zitachukua hatamu hivyo kwenye miaka mitano ya
utekelezaji shughuli zinazohimizwa na mafanikio yaweze kuingizwa ili
jamii ziweze kunufaika na misitu yao.
Naye
Afisa Uraghabishi na Mawasiliano wa TFCG Revocatus Njau amesema kwa
miaka miwili 2020 – 2021 TFCG inatekeleza mradi wa Haki Misitu kwa Kanda
za Kusini, Kasikazini na Nyanda za Juu Kusini na shughuli ya mradi huo
ni kuhamasisha kuhusu uhifadhi wa mistu ya vijiji, na kwamba tangu
kuanzishwa kwa sera na sheria ya misitu namba 14 ya mwana 2002 imeweza
kuleta mafanikio kwa vijiji zilivyorasimishwa na wanajamii wamekuwa
wakiitunza misitu yao kutokana na kupatikana na faida wanayoipata na
hiyo imeleta hamasa ya kuendelea kuhifadhi misitu.
“Lakini
hii ambayo haijahifadhiwa tumeendelea kuhamasisha kwa sababu misitu
ambayo haijaifadhiwa imekuwa na migogoro kwa sababu haina mpango wa
matumizi bora ya ardhi, hasa kwa migororo ya mipaka wafugaji na wakulima
na masuala mbalimbali ambayo maeneo yameingiliwa kutokana na kutokuwa
na mpangilio rasmi,”amesema Njau.
Meneja
Mradi wa Kuongeza Usimamizi wa Misitu ya Jamii katika misitu ya Pwani
amesema kwa kuangalia kiwango cha misitu ambayo haijahifadhiwa mradi
utawezesha jamii kwenye halmashauri ya Mtama kwa vijiji 10 kuweza
kuhifadhi na hekta kati ya 2,500 hadi 5,000 mpaka kumalizika kwa mradi
hiyo ni katika kupunguza hekta ambazo hazijahifdhiwa.
“Katika
uhifadhi huo tumeanza kusaidia jamii kufanya shughuli nyingine ili
kuwajengea utayari jamii kushiriki uhifadhi wa misitu ikiwemo ya
kuanzisha mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji na tumenza katika
kijiji cha Nteni,”amesema.
Yahaya
alisema jamii itasaidiwa kuweza kupima ardhi yao na itawezesha kila
kijiji kwenye vijiji 10 kupata hati miliki za kimila na kila kijiji
kitapata hati 150 sawa na hati 1500 kwa vijiji vyote kama sehemu ya
jamii kujifunza kwamba uhifadhi wa ardhi unawasaidia vyema kupata faida
moja kwa moja ikiwa ni pamoja na kupanda miti mbalimbali ya asili na
matunda ipatayo 20,000.
No comments:
Post a Comment