Jeshi la Polisi Wilaya ya Kilombero limeusambaratisha kwa mabomu ya machozi msafara wa Mgombea Mwenza wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana kupitia CHADEMA, Mhe. Salum Mwalimu, wakati mgombea huyo akisalimia wananchi waliosimamisha msafara wake Ifakara Mjini.
Polisi wakihakikisha msafara wa mgombea Mwenza wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana kupitia
CHADEMA, Mhe. Salum Mwalimu, unaondoka Ifakara bila ya kusimama njiani kwa lengo la kusalimia wananchi. Msafara huo ukiwa njiani polisi walilazimika kupiga mabomu ya machozi ili kutawanya wananchi waliosimamisha msafara wa mgombea huyo Ifakara Mjini.
No comments:
Post a Comment