Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro, amesema hayo leo katika ufunguzi wa mkutano wa vijana walio katika mtandao wa jumuiya za Umoja wa Mataifa nchini (YUNA) unaofanyika katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela jijini Arusha.
Amesema NMB ni benki inayothamini zaidi vijana na imejikita katika kutambua nafasi zao katika ujenzi wa taifa na ukuaji wa sekta ya fedha nchini.
Aikansia
amesema benki hiyo inaendesha programu maalumu kwa vijana wanaotoka
vyuoni–Graduate Trainee - kujifunza na baadae kupata kazi za kudumu, na
kati ya mwaka 2019 na
2020 zaidi ya vijana 50 wameshanufaika na programu hiyo.
“Tukiwa
tunatambua umuhimu wa mafunzo kwa vijana kabla ya ajira, kila mwaka
tunapokea vijana wenye sifa kuja kufanya mafunzo kwa vitendo huku
tukiwapa mikataba ya miezi mitatu
mpaka 12.
Pia tunapokea vijana kwaajili ya mafunzo wakiwa vyuoni yaani field attachment – na zaidi ya wanafunzi 300 wananufaika na mafunzo haya kila mwaka,” amesema Aikansia.
Mkutano
huo ulifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mwinyi Talib Hajj ambaye alitaka vijana
kutumia nafasi wanazopata
kujiendeleza kielimu ili kuwa na ushindani katika soko la ajira na fursa za ujasiriamali.
No comments:
Post a Comment