HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 18, 2020

RAIS MAGUFULI AWAAGIZA POLISI KUMUACHIA MKUU WA SHULE YA MSINGI BYAMUNGU ISLAMIC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais kupitia tiketi ya CCM Dkt. John Magufuli, ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani Kagera kumuachia Mkuu wa Shule ya Msingi Byamungu Islamic iliyopo Kata ya Itera wilayani Kyerwa mkoani Kagera wakati akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Gymkana Manispaa ya Bukoba.

 
 
Na Lydia Lugakila, BUKOBA
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea
urais kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Dokta
John Magufuli ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani
Kagera kumuachia mkuu wa shule ya Msingi Byamungu
Islamic iliyopo Kata ya Itera wilayani Kyerwa mkoani
Kagera anayeshikiliwa na jeshi hilo kufuatia tukio la moto
uliosabisha wanafunzi kumi kupoteza na wengine 7
kujeruhiwa baada ya bweni la wavulana kuwaka moto
usiku wa kuamkia Septemba 14 mwaka huu.
 
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo katika mkutano wa
kampeni uliofanyika katika viwanja vya Gymkana
vilivyopo mManispaa ya Bukoba ambapo amesema kuwa
wakati jeshi hilo likiendelea kufanya uchunguzi ni heri
kumwachia mkuu wa shule hiyo ili kumpunguzia mateso.

‘Bado hata akiwa nje ya maabusu nina uhakika
ataendelea kushirikiana na polisi katika kutoa taarifa, na
Ninafahamu mkuu wa shule ameshikiliwa na jeshi la
polisi inauma lakini mkuu huto wa shule nina uhakika
hakuwa na ubaya wa kuwachoma hao watoto kwa kuwa
aliwalea kama watoto wake, yeye alianzisha shule kwa
ajili ya watoto wetu kupata elimu kwa hiyo, ningeomba
sana aachiwe kwa sababu tunamuongezea mateso
mengine mbali na mateso ya kupotelewa na watoto wale
kumi alisema Rais Magufuli’’.
 
Aidha Rais Magufuli ameziagiza mamlaka zote husika
nchini ikiwemo wizara ya elimu elimu na wizara ya
TAMISEMI kuhakikisha shule zote hapa nchini
zinazingatia masuala ya usalama na sheria kabla na hata
baada ya kuanzishwa na hasa katika masuala ya ukaguzi
ili shule hizo ziwe zinazingatia matakwa ya kisheria ili
madhara hayo yasijirudie tena.
 
Rais Magufuli ameendelea kutoa pole kwa wanakgera na
watanzaia kwa ujumla na kuziomba familia
zilizopotelewa na watoto hao kuwa na moyo wa
uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Hata hivyo ikumbukwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti baada ya tukio hilo
aliagiza shule hiyo kufungwa kwa muda ili wanafunzi
wote warudi majumbani mpaka watakapoamriwa kurudi
tena huku serikali ikiahidi kugharamia mazishi ya wote
waliopoteza maisha pamoja na kuwatibu wote waliojeruhiwa. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake liimidiwe.

No comments:

Post a Comment

Pages