September 01, 2020

RC NDIKILO AWAWASHIA MOTO MA DC WALIOSHINDWA KUTEKELEZA AGIZO LAKE LA VITI NA MEZA


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wa pili kutoka kulia akiwa ameshika mkasi kujiandaa kukata utepe ikiwa ni  inshara ya ufunguzi wa makabidhiano ya viti na meza kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika Wilaya ya Rufiji wengine ni Mkurugenzi wa shirika la nyumbu pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na baadhi ya viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na wakuu wa idara katika halfa hiyo ya kukabidhiwa viti na madawati kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wilayani rufiji kuondokana na changamoto ya kukaa chini.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa amebega moja ya kitu ambacho kimetengenezwa na shirika la nyumbu lililopo wilayani Kibaha kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa shule ya sekondari na msingi wanaosoma katika shule mbali mbali za Wilayani Rufiji.

 

NA VICTOR MASANGU, PWANI

 

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka wakuu wa Wilaya za Mkoa huo ambao bado hawajatekeleza agizo lake la  kutengeneza madawati,viti pamoja na meza  kumpa malelezo ya kina  sababu zilizowakwamisha kutokufanya hivyo kwani lengo la serikali ni kuboresha sekta ya elimu na kuondokana na changamoto ya wanafunzi kukaa chini.

 

Akiongea wakati alikabidhiwa madawati na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Patrick Sawala mjini Kibaha, Ndikilo alisema agizo hilo alilitoa mwezi mmoja uliopita lengo likiwa ni kumaliza tatizo la watoto kukaa chini katika Mkoa huo.

 

"Wakuu wa Wilaya ambao hawajakamilisha kutengeneza madawati nipate maelezo ya kina yenye sababu za mashiko tujue kwanini hawajakamilisha hadi sasa" alisema Ndikilo.

 

Mkuu huyo alisema, Mkoa huo umejipanga kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa chini, ili wanafunzi wapate Elimu katika Mazingira bora .

 

" Tulikubaliana na Wakuu wa Wilaya katika kikao kazi tulichoketi mwezi mmoja uliopita hatuwezi kuwa na watoto wanaokaa chini na tarehe moja leo ndio ilikuwa mwisho" alisema.

 

Alisema, uwepo wa madawati ya kutosha shuleni itamsaidia mwanafunzi kuacha utoro, na mwalimu atakuwa anafundisha katika Mazingira mazuri .

 

Aidha Ndikilo aliwahimiza wakurugenzi kuacha kukimbilia kutengeneza madawati, Viti na meza kwa beii rahisi na badala yake kwenda sehemu ambazo zinamatengenezo yenye ubora . 

 

" Madawati haya yanayotengenezwa hapa katika shirika la Nyumbu ni tofauti na mitaani, yanauwezo wa kudumu kwa miaka mitano tofauti na huko mtakakoenda ambako kila mwaka mtakuwa mnatenga bajeti kukarabati au kutengeneza upya" alisema

 

 Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Dr Delphine Magere alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Rufiji kwa kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa kwa wakati.

 

Alisema Kauli mbiu ya Pwani hakuna kukaa chini itatekelezwa kwa vitendo kwani Mkoa huo ni wapiganaji wanaopigania nchi na kwahivyo nchi itakuwa na wasomi wakupeleka uchumi mbele.

 

Akimkabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa Mkoa , Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Patrick Sawala alisema, Wilaya hiyo ilikua na mapungufu ya meza 1882, Viti 231 na madawati 3945 na kwamba wamejipanga kuhakikisha wanatekeleza mpango huo.

 

Alimshukuru Mkurugenzi wa Shirika TACT Nyumbu kwa kumaliza matengenezo ya Viti na meza 300 kwa wakati.

 

Mkurugenzi wa Shirika TACT Nyumbu Brigedia General Hashimu Komba alisema, mwitikio ni mkubwa kwa watendaji kuitikia agizo la Mkuu wa mkoa kutumia Shirika hilo kutengeneza madawati, Viti na meza zinazohitajika.

No comments:

Post a Comment

Pages