NA JANETH JOVIN
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limefanya ukaguzi wa bidhaa ambazo hazijathibitishwa katika Soko la Kariakoo na kukutana na baadhi ya vipodozi ambavyo vinatajwa kuwa na viambata sumu.
Akizungumza wakati akiongoza zoezi hilo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile amesema kuwa katika soko hilo la Kariakoo wamekuta vipodozi venye viambata sumu na haviruhusiwi kuuzwa hapa nchini.
Amesema TBS wataviondoa vipodozi hivyo sokoni na wahusika watachukuliwa hatua za kisheria kwa kosa hilo la uzaaji wa vipodozi vyenye viambata sumu.
"Tangu Julai mwaka jana, shirika limekuwa likifanya usajili wa bidhaa za vipodozi na vyakula ili kuhakikisha zinapokwenda sokoni au kuhifadhiwa ziwe katika mahali salama na kwamba hakuna madhara yeyote yanayoweza kutokea kutokana na uhifadhi au utumiaji wa bidhaa hizo.
" leo katika soko hilo la Kariakoo tumekuta vipodozi venye viambata sumu na haviruhusiwi kuuzwa hapa nchini, hivyo basi TBS tutaviondoa na wahusika wote watachukuliwa hatua zinazostahili," amesema
Amesema kuwa wahusika hao wamekuwa wakiuza bidhaa hizo kinyemela na sio kwamba hawaelewi utaratibu wanaotakiwa kuufuata wa kusajili bidhaa zao na maeneo wanayohifadhia.
"Watu hawa wamekuwa wakikiuka taratibu hizo na sisi hatuwezi kukaa kimya ndio maana tumekuja hapa kuviondoa ili kuhakikisha soko la Tanzania linakuwa na bidhaa bora na usalama," amesema
Naye Mtathimini na Msajili wa bidhaa za vipodozi kutoka TBS, Ambumi Mwapeta amesema wataziharibu bidhaa zote hizo walizozikamata na kuongeza kuwa anatoa wito Kwa wauzaji wa vipodozi kwenda TBS Kwa ajili ya kuzisaji na kupewa maelekezo mengine ya kitaalam juu ya bidhaa zinazopaswa kuwepo sokoni.
September 07, 2020
Home
Unlabelled
TBS yakamata vipodozi vyenye viambata simu Kariakaoo
TBS yakamata vipodozi vyenye viambata simu Kariakaoo
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment