September 04, 2020

UJUE UWEKEZAJI KATIKA MFUKO WA HATI FUNGANI

 

Na Mwandishi Wetu

 

UWEKEZAJI wa Pamoja unaweza kuwa kitu kipya kwa Watanzania wengi japo Kampuni ya Uwekezaji (UTT AMIS) imekuwepo tangu mwaka 2005 ikihamasisha uwekezaji wa aina hiyo.

 

Katika nchi nyingine duniani, uwekezaji wa aina hiyo umekuwepo muda mrefu. 

 Kwa mfano, India Unit Trust of India imekuwepo tangu mwaka 1963.

India Unit Trust of India ni kampuni ya serekali, ilikaa sokoni kwa miaka 24 bila mshindani ndipo zikaanza kuanzishwa kampuni binafsi za Uwekezaji wa Pamoja.

Hadi sasa, kuna kampuni zaidi ya 2,500 za Uwekezaji wa pamoja. Nchini Marekani kuna kampuni zaidi ya 10,000 zote zikijaribu kuwavuta wawekezaji ili washiriki kwenye  uwekezaji huo wenye mafanikio makubwaa duniani.

Mifuko ya Uwekezaji wa pamoja iko aina mbalimbali ili kukidhi malengo ya wawekezaji. Wapo wawekezaji ambao wanataka kipato cha mara kwa mara.

Wengine wanataka kukuza mtaji, elimu kwa watoto, uwekezaji na bima mfano ya maisha au ulemevu wa kudumu, kipato ndani ya muda mfupi na malipo kwa haraka zaidi.

Mifuko hiyo ipo inayowekeza kwenye hisa, hati fungani,  kwenye benki lakini iko mingine haiwekezi kwenye hisa, inawekeza kwenye hati fungani tu na kwenye bidhaa za benki mfano Mfuko wa Hati Fungani wa UTT AMIS.

Mtu mwenye nia ya kuwekeza kwenye Hati Fungani anaweza kushawishiwa kwenda kununua hati fungani sokoni badala kununua kupitia Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja uliosimamiwa na UTT AMIS.

Mwekezaji anaweza kuwa sahihi lakini anaweza kukosa faida zifuatazo. Mfuko wa Hati Fungani wa UT AMIS ni njia mpya ya uwekezaji katika Uwekezaji wa Pamoja ambayo awali haikuwepo nchini.

Siku za nyuma mtu binafsi au kampuni mbalimbali zilikuwa zikienda moja kwa moja kununua hati fungani za muda mfupi au mrefu.

Hivi sasa inawezekana watu, makundi mbalimbali, kampuni na serekali hukusanya fedha zao pamoja chini ya Meneja UTT AMIS ambaye ataziwekeza fedha hizo kwa niaba yao na kila mtu kupata faida au hasara kama itakuwepo japo.

Katika hali ya kawaida, huo ni uwekezaji salama kwa kampuni iliyopo chini ya serikali lakini uwezo wa kampuni binafsi kulipa ni mdogo sana.

Ni vigumu mtu binafsi kuwa na fedha za kutosha ili kunua hati fungani ya kampuni binafsi ila kwenye Uwekezaji wa Pamoja, kwa kuwa fungu la pesa ni kubwa, Meneja UTT AMIS anaweza kuwekeza alimia 8 kwa kampuni binafsi, asilimia 92 hati fungani za serekali za miaka tofauti.

Kupitia Mfuko wa hati Fungani, si lazima uwe tajiri ili kuwekeza katika hati fungani, unaweza kuanzia sh. 5,000 ambazo zitatosha kuanza kunua hati fungani baada ya kipindi cha zuio kuisha.

Hii ina maana kuwa, hata yule mwenye kipato kidogo ana nafasi ya kuwekeza. Kwa kufanya bei kuwa ndogo kuna vuta mtaji mkubwa wa kuwekeza.

Mtaji ukiwa mkubwa maana yake nguvu ya majadiliano inakuwa kubwa na gharama za uendeshaji zinakuwa ndogo, hii ina maana kuwa wigo wa faida unaongezeka.

Wenye mtaji mdogo wanafaidi na punguzo la gharama linalopatikana kupitia uwekezaji wa pamoja.

Ujuzi tofauti kwenye hisa mfano kuwekeza kwenye hati fungani kuna hitaji uchunguzi bobezi zaidi mfano kujuwa uwezo na tabia ya anayeuza anayeuza hati fungani.

Hata kama ni serekali hali ya kiuchumi ikoje, tegemeo la baadae likoje mfano thamani ya fedha, mfumuko wa bei, mambo mengine muhimu kama riba .

Hati Fungani daima ni tulivu ikitoa fursa ya kujikinga na kujijenga.

Kwanini uwekeze katika Hati Fungani? Katika dunia ya sasa, hati fungani inawakilisha uwekezaji usio na mawimbi makubwa. Wakati hisa zinatawala vichwa vya habari, hati fungani inawalinda na mdororo wa uchumi.

Hati fungani huwa ni kimbilio lao kwani mara nyingi bei ya hati fungani inakwenda kinyume na riba zake.

Ni ukweli usiopingika kuna wakati hisa zinalipa sana lakini ni rahisi kutabiri mwenendo wa hati fungani ukilinganisha na ule wa hisa.

Uzuru wa hati fungani ni kwenye uhusiano wake na uchumi, wakati nchi inataka kuendeleza miradi zaidi inahitaji pesa, pia wakati uchumi unadorora pesa zinahitajika ili kuuweka sawa, hati fungani kila wakati imekuwa kati ya jawabu la uhakika.

Mara nyingi uwekezaji unategemea malengo, muda na uvumilivu wa hali hatarishi ambatanishi.

Umri unaenda, mahitaji  ya kipato cha mara kwa mara yanakuwa makubwa hivyo Mfuko wa Hati Fungani ndiyo suluhisho ukisonga mbele na hausimami.

KUINUA KIPATO

Kwa kawaida, hati fungani za serekali zinalipa faida kwa uhakika sana lakini faida yake mara nyingi ni ndogo ukilinganisha na hati fungani za kampuni.

Ili kupata kipato kizuri unashauriwa kuchanganya hati fungani za kampuni binafsi na serekali.

Kuna kampuni binafsi zingine hazina historia kama ziko kwenye misingi mizuri ya kuweza kuwekeza. Kimsingi unapaswa kuchukua tahadhari  kubwa.

Mambo yakiwa mazuri faida inakuwa kubwa ila yakienda mrama huzuni inaweza tawala. Kampuni zisizoaminika zinaweka riba nzuri ili kuvuta wawekezaji.

Hati fungani za muda mrefu zina unafuu wa kodi. Hii ni nzuri kwa mwekezaji kwani ina muhakikishia kipato zaidi.

Tukumbuke kuwa, ukinunua hati fungani ina maana  umekopesha fedha zako kwa serekali kama hati fungani hiyo ni ya serekali pia kwa kampuni kama hati fungani hiyo ni ya kampuni kwa muda maalum na riba iliyokubaliwa.

Tukumbuke pia mwekezaji anaweza kunua hati fungani moja kwa moja, hii inakuwa rahisi kama mtaji ni mkubwa, pia awe anaweza subiri kupata gawio kila miezi sita, awe mwingi wa subira ya kupata mkopo.

Hati fungani zipo za miaka tofauti. Pia tukumbuke kuwa, mwekezaji anaweza uza hati fungani yake kama atahitaji pesa zake na atauza akipata mnunuzi.

Kwenye Mfuko wa Hati Fungani (Bond Fund) unaweza kuwekeza kiasi kidogo cha mtaji na kupata gawio mara kwa mara, si lazima usubiri mizi sita, utauza hati fungani yako muda wowote bila shida.

Ukinunua hati funagani moja kwa moja unapata faida kama mlivyokubaliana yani kama kila miezi sita asilima 7 itakuwa hivyo na asilimia iliyokubaliwa baada ya muda kuisha itakuwa hivyo pia.

Lakini ukinunua kupitia uwekezaji wa pamoja itategemea thamani ya kipande hivyo mwekezaji ata faidi thamani ya kipande iko juu, ikiwa ndogo faida inaweza kupungua.

Badilika, chukuwa hatua, wengi tunatamani kuwa matajiri, wengi tunatamani fedha zao ziwe nyingi zaidi lakini woga ndiyo shida yetu.

Waswahili wanasema woga wako ndiyo umaskini wako, Watanzania wengi hawapendi kuthubutu, wanaogopa.

Kumbuka hakuna maajabu duniani, lazima tuwekeze ili kuongeza kipato chetu. Wengi wetu tuna pesa zimekaa tu nyumbani au benki bila kufahamu fedha hizo tungezipa thamani zaidi kwa kuziwekeza sehemu salama kama  kwenye Mfuko wa Hati Fungani.

Wale waoga wa kuwekeza hupenda kupitia kwenye mifuko ambayo ni salama sana. Unaweza kupata faida lakini itakuwa ya wastani.

Ili upate faida kubwa ni muhimu kuwekeza sehemu zenye hali hatarishi kidogo. Mfano mifuko inayochanganya hati fungani na hisa. Hisa ni chachu ya faida pia ni chachu ya hasara. Mara nyingi Hati Fungani zitakupa faida  ambayo mara chache sana yaweza kuwa zaidi ya asilimia 15-16.

Mara nyingi maamuzi ya wapi uwekeze yanaendana na malengo, umri, muda, faida tarajiwa. Kwa mfano, mtu anayekaribia kustaafu ataridhika na faida ya wastani.

Hata penda kuwekeza sehemu ambayo ni hatarishi kwani pengine hana nguvu ya kuhangaika tena ili kutafuta. Hicho alicjhonacho kinaweza kuwa turufu yake ya mwisho.

Kwa vijana wanaweza kuthubutu kwani wana muda wa kuanguka na kusimama kwa nguvu zaidi. Wana muda wa kujifunza kutokana na makossa yao.

Siku hizi kuna usemi unaosema,  jifunze kutokana na makossa ya wenzio, usisubiri mpaka uanguke ndio ujifunze kutokana na makosa yako.

Malengo yanaweza kukufanya uwe na msimamo wa woga mfano mtu anayeweka fedha ili kununua nyumba, ada ya shule ni tofauti na mtu anayewekeza ili kwenda kutalii.

Nyumba na ada ya shule ni lazima lakini kutalii si lazima. Pesa ya nyumba na ada ya shule unaweza kuiweka katika hali ambayo si hatarishi sana.

Pesa ya utalii unaweza kuiwekeza katika mradi ambao una viashiria vya hatari zaidi ambavyo vikienda sawa vinakupa faida nzuri zaidi.

Kwa mwekezaji mwenye malengo ya muda mrefu anaweza anza kuwekeza sehemu ambayo inaweza kumpa faida sana au sehemu ambayo faida tarajiwa ni kubwa sana huku dhoruba zake zikiwa juu kama zitatokea.

Kadri muda na lengo lako linavyokaribia, unaweza kuhamisha uwekezaji katika maeneo yenye hatari za uwekezaji kidogo na faida za wastani.

Uli uweze kupata ufanisi ushauri ni muhimu, unaweza kutembelea Ofisi za UTT AMIS, Introduction.

Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja inazidi kuwa maarufu unaotokana na urahisi wa kuwekeza, uwazi katika kupata taarifa,  uhimili wake kwenye hali hatarishi.

Hiyo ni pamoja na ukweli kuwa, lazima isimamiwe kwa mfano, Tanzania msimamizi ni Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSCA), mwangalizi ni Benki ya CRDB.

Uzuri wa mifuko hiyo, huudumia mwekezaji mwenye fedha nyingi ama kidogo, wote wanapata huduma sawa kiutaalamu.

Fedha chache huchanganywa na fedha nyingi na kuwa fungu moja . Ukiwekeza kwenye vipande unaweza uza, kunua vipande wakati wowote isipokuwa kwa baadhi ya mifuko mfano kama ile yenye faida pacha, uwekezaji na huduma za bima.

Faida ni nyingi lakini changamoto zipo pia kubwa ni thamani ya kipande inaweza kupanda au kushuki.

Watanzania wengi bado wanaamini benki ndiyo sehemu pekee na sahihi ya kutunza pesa, pia si Watanzania wote wanaojuwa benki ni chombo pekee wanachoweza kukitumia kama daraja la uwekezaji.

Mfano, ukiwa na pesa katika akaunti yako ya akiba, tunasema kuwa pesa hiyo umeiweka, umei tunza lakini ukiwa na pesa kwenye akaunti ya muda maalumu, pesa hiyo inakuwa imejiwekeza.

Katika kuitunza pesa na kuiwekeza kwenye akaunti za muda maalumu mara nyingi muhusika anajuwa atapata nini mwisho wa siku lakini kwenye Uwekezaji wa Pamoja ni ngumu kujuwa mwisho wa siku utapata kiasi gani.

Kipato kinategemea mrejesho wa pesa zako zilipowekezwa  ila unaweza kuelezwa ni kiasi gani cha chini kulingana na malengo ya sera za mfuko husika.

Jambo la muhimu kwa mwekezaji ni kuangalia historia ya Kampuni ya Uwekezaji wa Pamoja, kufanya tathmini ya utendaji wake wa nyuma japo haukupi uhakika wa utendaji wa siku za mbele.  

Tathmini nyingine zitakufanya uweke au uwe mwekezaji  kupitia chombo kipi. Mara nyingi uwekezaji katika mifuko ya pamoja hukupa faida shindani ziadi ukilinganisha na uwekezaji katika benki, hati fungani za muda mfupi.

Mifuko mingine inayosimamiwa na UTT AMIS ni Mfuko ya Umoja, Wekeza Maisha, Watoto, Jikimu, Ukwasi, yote imeanzishwa kitaalamu sana katika misingi thabiti ya kishera inayomuhakikishia mwekezaji kuwa pesa zake zitakuwa salama.  

Menejimeti, Bodi, mwangalizi na wadau wengine akiwemo CMSA wanafanya kazi pamoja kuhakikisha mwekezaji hapewi taarifa za uongo, uwekezaji ake uko salama na ulinzi imara kwa ujumla.

Kila mfuko una waraka wa makubaliano ukiainisha haki ya mipaka ya kampuni ya uwekezaji wa pamoja, wawekezaji, na wadhamini.  

Ni seti ya taratibu zitakazofuatwa kuhakikisha kila upande unapata haki zake, vitu kama uwiano wa uwekezaji, manunuzi na malipo ya vipande, gharama za kujiunga na kutoka katika mfuko, haki zingine vimeainishwa bayana ili kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri.

Kampuni inayofanya Menejimeti ya fedha za wawekezaji inakuwa tofauti  na mifuko kwa maana ya kuwa na Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti yake, hesabu zake ambazo havihusiani na mifuko.

Kazi yake ni kusimamia ,kuendesha mifuko ya uwekezaji kwa tozo iliyokubaliwa.  Kazi ya kampuni hii ni kutangaza, kuiuza mifuko, kuratibu, uuzaji vipande, kuweka kumbukumbu muhimu za kibiasha, kuwekeza kitaalamu.

UTT AMIS mbali ya kusimamia mifuko hiyo pia inatoa huduma ya usimamizi, uangalizi wa mali kwa watu wenye kipato kikubwa.

Wawekezaji wananunua na wanamiliki vipande. Ukiwa mwekezaji unakuwa sehemu ya uwekezaji lakini huwezi sema una miliki mfuko.

Meneja wa UTT AMIS anawekeza vipande vya mwekezaji kitaalamu,  kenye masoko ya fedha na mitaji. 

Bei ya vipande kwenye mfuko mmoja ni sawa, tofauti kwa wawekezaji inakuwa idadi ya vipande kwani nguvu ya fedha kati ya mwekezaji mmoja na mwingine ni tofauti.

Anayewekeza fedha nyingi anapata vipande vingi zaidi, vipande vina viwango vya chini vya manunuzi lakini hakuna ukomo wa kiwango.

Kila mwekezaji anatapata faida sambamba na idadi ya vipande vyake, kwa kawaida faida ya kipande ni ile ile ila mwenye vipande vingi anavuna zaidi kuliko mwenye vipande vichache.

Je, kuna uhakika wa mapato kwenye uwekezaji wa pamoja, kama maelekezo ya Mamlaka ya Masoko ya dhamana na Mitaji, thamani ya kipande inaweza kupanda au kushuka.

Uwekezaji huo hauna tofauti na biashara ya duka au hoteli, huwezi kupata faida sawa kila siku,  lazima kiwango cha faida kitofautiane siku hadi siku na pengine hata hasara inaweza kutokea.

Hasara inaweza kuletwa na mabadiliko katika hali ya soko, utendaji mbaya wa kampuni inayosimamia, hasara.

Hayo yote huzingatiwa kwa umakini mkubwa na UTT AMIS inayowekeza sehemu ambapo viashiria vya hasara vimechunguzwa kwa umakini, umahiri wa hali ya juu na ndiyo sabubu kubwa ya wawekezaji kuongeza Imani na kuwekeza zaidi na zaidi.

Hadi sasa, UTT AMIS inasimamia zaidi ya sh. bilioni 300, katika nchi nyingine duniani, kampuni za uwekezaji wa pamoja zinawekeza zaidi ndani ya nchi.

Tanzania ambako iko kwenye hatua za mwanzo kutokana na uchache wa kampuni za aina hiyo tofauti na nchi nyingine zilizoendelea kama Marekani, unakuta kuna kampuni zaidi ya 10,000, India zaidi ya 2500.

Nchini India, Unit Trust of India ilianza mwaka 1963 ikiwa ni kampuni ya Serekali, baada ya miaka zaidi ya 20 ndipo kampuni binafsi zikaingia kwa kasi.

Kasi hiyo inaonyesha kuwa, uwekezaji wa pamoja ni njia sahihi katika ukombozi wa maisha yetu ya sasa na baadae.

Kwa sasa UTT AMIS inakaribisha wawekezaji kutoka nchi za Afrika Mashariki na baadhi ya mifuko kama huo wa Hati Fungani, wawekezaji kutoka dunia yote.

Zipo kampuni ambazo zinawekeza ndani kidogo  kwa mfano kama asilimia 15 huku asilimia zaidi ya 85 ikiwaa ni uwekezaji kwenye masoko ya nje katika nchi nyingine.

Pia kuna kampuni kubwa na ndogo uwekezaji wake ukiwa kwenye hisa zaidi, nyingine kwenye mikopo zaidi (hati fungani na akiba maalumu benki), zingine zikiwa kwenye mchanganyiko yaani hisa na mikopo.

Busara ni kwa mwekezaji kuchukuwa hatua sasa na kuanza kuwekeza kidogo kidogo japo hisa zina mawimbi lakini tukizingatia muda mrefu, uwekezaji kwenye mifuko ya hisa au yenye sehemu ya hisa imekuwa ikilipa zaidi ya ile isiyo na hisa au si ya uwekezaji wa hisa.

Hisa katika muda mrefu zimekuwa zikilipa zaidi ya hati fungani na akiba za muda maalum (fedha) katika hali ya kawaidi.

Kwa wawekezaji wajanja ni vizuri kuanza kuwekeza mapema, kuwa na malengo ya muda mrefu ili ukistaafu uwe unakula gawiwo huku mtaji wako ukiwa pale pale.

Hii ni kwa sababu utakuwa umewekeza mara kwa mara na utakuwa umepata faida jumuishi. Changamoto ni wawekezaji wengi kuwa na mambo mengi.

Wengine wana madeni mbalimbali, ada za watoto, matibabu ya watoto, familia nzima, chakula, malazi, mavazi na mambo mengine kemkem.

Kwa sababu ya shida hizo, wanachelewa kuwekeza wakati siku zikiendelea kusonga mbele, wanachelewa kuanza lakini ndege ya uwekezaji haisubiri.

Ukichelewa kuanza unapunguza muda wa kuwa mwekezaji, muda ni silaha ya kupambana na dharuba katika masoko.

 

Kila mtu ana kila sababu ya kuwa mwekezaji, ukiwekeza fedha zako unazipa nafasi ya kukua, hakuna mtu asiyependa kuwa na maisha ybora.

Hakuna mtu asiyependa kuongeza pesa alizonazo, njia bora kabisa ya kuongeza pesa hizo ni kuwekeza kwa makini na umakini unapatikana kwa wataalamu waliobobea kama UTT AMIS.

Kwa kila tunalofanya tukumbuke kuwa, kuna maisha ya baadae hasa baada ya kustaafu. Pamoja na biashara zingine kama usafiri, nyumba, ufugaji, kilimo ni vizuri ukawekeza kwenye sehemu kama hisa, hati fungani hata kwenye akaunti za muda maalumu.

Baada ya kustaafu utaishi kwa pesa ulizowekeza ambazo zitakusaidia zaidi kutokana na akiba uliyoiweka.

Kwa mfano, kama kukiwa hakuna mabadiliko, ukiweka 400,000 kila mwezi, asimia 12 kwa miaka 10 utakua umeweka sh. milioni 48 lakini utapata zaidi y ash. milioni 92 kwa kipindi hicho kama riba asilimia 12.

Hapa UTT AMIS imezingatia kuwa, thamani ya kipande inaweza kupanda au kushuka ndiyo maana wanakadiria faida asilimia 12 . Mfano huo utakuwa na uhalisia kama hakuna mabadiliko katika daraja za uwekezaji.

Ili upate faida kubwa ni veme uanze kuwa mwekezaji mapema na pengine mjasiri kidogo kwenye uwekezaji.

Umri unapozidi kuwa mkubwa unapoteza hamu ya kuthubutu kuwekeza sehemu zenye mawimbi mazito, hatarishi ila tukumbuke usemi unaosema; “The higher the risk, the higher the profit”.

Tukumbuke kuwa, UTT AMIS ina mifuko inayoendana na matakwa ya mteja, ipo yenye mawimbi makubwa, ya kati na madogo yote ikitoa faida kwa wawekezaji.

Uwekezaji ndiyo njia muafaka ya kufanikasha malengo yako kama kununua gari, kujenga nyumba, kuanzisha bisharana kusomesha watoto.

UTT AMIS inawakaribisha wananchi wote kupata elimu inayohusu uwekezakji wa pamoja, kumbuka hadi sasa ina mifuko sita ya uwekezaji ukiwemo wa Hati Fungani.

Pia kampuni hiyo inatoa huduma ya usimamizi wa mali kwa wateja wenye ukwasi mkubwa. Ukiacha huduma hiyo mifuko yote ya UTT AMIS inafaa kwa kila mwananchi bila kujali kipato chake ni kikubwa au kidogo.

Jamii inakumbushwa kuwa, mfuko mpya wa Hati Fungani ama Bond Fund, unaendelea kuuza vipande hivyo ni wakati mzuri wa kuchangamkia fursa hiyo. Thamani ya kipande unaweza kupand au kushuka.

No comments:

Post a Comment

Pages