September 05, 2020

UNIVERSITY ABROAD WAVIPA MCHONGO VYUO VIKUU NCHINI

Na Mwandishi Wetu


MKURUGENZI wa Kampuni ya University Abroad Representative (UAR) Tanzania  Tony Kabetha, ametoa wito kwa vyuo vikuu nchini kutumia vema kampuni yao kupata wanafunzi kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.

 

Kabetha ametoa wito huo leo katika maonesho ya 15 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


“Sasa umefika wakati vyuo vyetu vikuu kutumia fursa ya kampuni kama sisi (University


Abroad Representative) kuwaletea wanafunzi kutoka nje kama ambavyo vyuo vikuu Duniani vinatutumia sisi kupata wanafiunzi kutoka hapa nchini.


“Kama vyuo vikubwa duniani kutoka maiafa makubwa vimetuamini kwa ushindani wetu na tunafanya navyo kazi nadhani ni wasaa sahihi kwa taasisi za hapa nchini kunufaika na uwepo wetu kupata wanafunzi wanaotoka nje ya mipaka ya nchi, jambo ambalo litakuwa na faida ya kiuchumi lakini pia kulijengea taifa letu heshima Kimataifa.”amesema Kabeta.

 

Aidha amesema Kampuni yao imejipanga vilivyo kwa ajili ya kuendelea kuwafungulia milango vijana wa akitanzania wanaohitaji kupata Elimu nje ya mipaka ya nchi wanafanikiwa kwa wakati na kwa ubora Zaidi.

 

 

 Baadhi ya wanafunzi wakipata ufafanuzi wa namna ya kujiunga na vyuo vikuu vya nje walipotembelea banda la Kampuni ya University Abroad Representative (UAR) katika Maonesho ya 15 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

 

Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,  Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo (katikati) akiwa katika picha ya kumbukumbu na washiriki wa maonesho hayo. 

Mkurugenzi wa Kampuni ya University Abroad Representative (UAR) katikati akiwa katika picha ya kumbukumbu.


No comments:

Post a Comment

Pages