Mgombea wa Ubunge wa
jimbo la Mkuranga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdallah Ulega, akihutubia mkutano wa kampeni jimboni kwake.
Baadhi ya wakati wa jimbo la Mkuranga wakimsikiliza mgombea ubunge wa jimbo hilo.
MGOMBEA wa Ubunge wa jimbo la Mkuranga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdallah Ulega amewaomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua na kukichagua chama hicho, ili pamoja na mambo mengine aweze kutekeleza miradi mbalimbali iliyopo katika jimbo hilo.
Akizungumza katika mikutano mbalimbali ya hadhara anayoendelea kuifanya katika jimbo hilo, Ulega alisema mikakati aliyonayo endapo atachaguliwa ni kuhakikisha anaipaisha Mkuranga kimaendeleo kama ambavyo ilani ya CCM ilivyokusudia kufanya hivyo nchi nzima.
Akiwa katika Kijiji cha Chatembo, Mgombea huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, aliahidi ujenzi wa shule ya msingi Chatembo baada ya kupata ekari 15 kutoka serikalini katika msitu wa unaomilikuwa na Wakala wa Misitu Tanzania(TFS)
Pamoja na shule hiyo pia Ulega alisema endapo wananchi hao watamchagua atahakikisha anaijenga barabara kutoka Bakhresa hadi Chatembo na Mwembemtengu hadi Lugwadu kwa kuwa tayari barabara hizo zimesajiliwa na TATURA.
Mbali na hilo pia amehadia suala la upanuzi wa barabara ya Kilwa kutoka Mbagala Rangitatu hadi Mwandege sambamba na ujenzi wa kituo cha cha kisasa cha mabasi katika kijiji hicho cha Mwandege.
Aidha aliitaja miradi ambayo aliitekeleza katika kipindi cha 2015/2020 kuwa ni pamoja na Ujenzi wa shule za msingi Juhudi katika kijiji cha Kipala Mpakani na shule ya msingi Lugwadu katika kijiji cha Lugwadu, ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Mkokozi pamoja na Ujenzi wa shule ya Sekondari ya Mwandege.
Pamoja na hiyo pia alisema masuala mengine aliyoyasimamia ni pamoja uunganishaji wa umeme katika vijiji vya Lugwadu na Mkokozi pamoja na vitongoji vya Chatembo,Vicheji,Mwemanani,Mseru.

No comments:
Post a Comment