Na Asha Mwakyonde
VIJANA na wataalamu wa makumbusho wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utafiti lengo likiwa ni kuwapatia mbinu mpya za uhifadhi wa mali za kale.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Agosti 7, mwaka huu wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu Rasi wa Ndaki ya Insia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Rose Upor, amesema mafunzo hayo ni mradi mkuu wa utafiti ulifadhiliwa na tà asisi mbalimbali za vyuo.
Amezitaja taasisi hizo kuwa ni makumbusho ya ujerumani ya ujerumani Ethinelico missio na chuo kikuu Humboji cha Ujerumani na chuo kikuu cha Dar es Salaaam cha Tanzania idara ya historia.
Amesema Makumbusho ya Taifa itaendelea kushirikia na wadau mbalimbali kusaidia makusanyo yaliyopo kwenye makumbusho hayo Dkt. Rose ameongeza kuwa mwisho wa mafunzo hayo wanatarajia wataalamu hao watatumia ujuzi huo kufanyakazi kwa ufanisi mkubwa na kuupeleka ujuzi huo kwa wengine ambao hawajashiriki warsha hiyo.
Naye Mkurugenzi Mkuu makumbusho ya taifa Dkt. Noel Lwoga amesema mafunzo hayo ya kujenga uwezo wa vijana wawezo kufasiri baadhi ya nyaraka zilizopo makumbusho na kubaini sayansi iliyotumika kupata makusanyo na kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.
Kwa upande wake Mratibu wa warsha hiyo muhadhiri mwandamizi wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Oswad Masebo, amesema tafiti zinazofanywa ni kupitia makusanyo zilizopo kwenye makumbusho ili kubaini asili ya nchi,ujenzi wa Taifa na maendeleo ya nchi wapi tulipotoka na tunapikwenda .
No comments:
Post a Comment