Na Lydia Lugakila, BUKOBA
Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally, amewataka watanzania kuwa na mshikamano ili kuwakwepa watu
wenye nia mbaya wanaotaka kuigawa nchi katika vipande vipande alivyoviita majimbo.
Dokta Bashiru ametoa kauli hiyo katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Gymkana vilivyopo manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Amesema kuwa Katika karne ya 21 wapo watu wanaopanga kuwa wakichaguliwa na kuingia ikulu wataigawa nchi katika mapande yaitwayo majimbo ambapo ameyataja majimbo hayo kuwa ni pamoja na kila jimbo kubeba reli yake kila jimbo kusomesha watoto wake kila jimbo kujenge hospitali yake jambo ambalo amesema kuwa ni sera zilizofirisika.
Aidha Amesema kuwa Rais Magufuli anafanya kazi kubwa
ya kuliunganisha taifa na afrika nzima. ‘’Kizazi chetu hatuwezi kuzungumza sera za majimbo sera za kikoloni tunajenga bomba refu la mafuta kutoka Tanga hadi Uganda tunaiunganisha afrika wenzetu.
wanataka uongozi wa kuwagawa watanzania katika
vipande vipande maarufu majimbo. ‘’Tunajenga reli ya mwendokasi kuiunganisha Tanzania tunayo reli ya Tazara inaunganisha afrika tunajenga viwanja vya ndege kuiunganisha Tanzania na dunia alisema katibu huyo.’’
Amesema kuwa Watu waliofirisika kisiasa wanapanga
kuikata kata Tanzania katika vipande vipande viitwavyo majimbo na kila jimbo kuwa na mtawala anayeitwa Gavana jina aliloliita kuwa ni la kikoloni.
Hata hivyo amesema kuwa ni muda sasa kwa watanzania
kutokubali mfumo wa namna hiyo kwa kuwa mwalimu
nyerere alisifika kwa kuongoza mapambano ya ukombozi
wa bara la afrika huku akiwaomba watanzania kuwa na mshikamano utakaowavusha
No comments:
Post a Comment