HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 02, 2020

KOKA APANIA KUWAONDOLEA CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA VIFAA TIBA WANANCHI WA KIBAHA MJI

Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kibaha Mjini, Sylvestry Koka kupitia CCM akizungumza na baadhi ya  wananchi wa kata ya Maili Moja ikiwa ni moja ya kampeni zake kwa ajili ya kuomba ridhaa kwa wananchi waweze kumchagua tena katika kuongoza katika kipindi cha miaka mitano mingine.

 

 

VICTOR MASANGU, KIBAHA

 

Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha mji kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) Sylvestry Koka amesema endapo atachaguliwa na wananchi kuwaongoza tena katika kipindi kingine cha miaka mitano atahakikisha analivalia njuga  suala la kukabiliana na changamoto  inayowakabiliwa  wakinamama wajawazito kupoteza maisha wakati wa kujifungua  kwa  kuboresha sekta ya afya ikiwemo  kununua vifaa tiba vya kisasa.

Koka aliyasema  hayo wakati wa kampeni ya kuomba kura kwa wananchi wa maeneo ya mbali mbali ya bundikani katika  kata ya Maili moja ambapo amebainisha kwamba nia yake kubwa ni kuendelea kushirikiana na wananchi na serikali ambayo itaingia madarakani katika kuweka mazingira rafiki katika utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi husussan wakinamama wajawazito.

Ndugu zangu wananchi pamoja na kuwepo kwa mambo mbali mbali ya kimaendeleo ambayo nimeshakwishayafanya lakini tumekuwa na mradi mwingine wa Kijimbo ambapo tumeweza kushirikiana na serikali kwa kujenga jengo kubwa la kisasa  kwa ajili  ya kujifungulia wakinamama ambalo limejengwa pale katika hospitali teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani tumbi haya ni moja ya juhudi zangu katika kuboresha afya,”alisema Koka.

Aidha mgombea huyo alibainisha kwamba kutokana na kuwepo na changamoto ya upatikanaji wa wa utoaji wa huduma katika baadhi ya maeneo alipambana vilivyo mnamo mwaka 2012 kwa ajili ya kuomba ujenzi wa mradi wa hospitali mpya ya Wilaya ambapo maombi yake yaliweza kuzaa matunda kutokana na mradi huo kukamilia.

“Wakati nipo katika nafasi yangu ya Ubunge mnamo mwaka 2012 niliomba ujenzi wa hospitali ya Wilaya lakini alivyoingia katika kipindi kingine aliweza kupambana kutokana na kuona kuna umuhimu mkubwa wa hospitali hiyo ambayo itaweza kuwa mkombzo mkubwa kwa wananchi kupatiwa matibabu yao kwa urahisi  na kwamba kwa sasa hospitali hiyo imekamilika na tayari imeshaanza kutoa huduma,”alisema Mgombea huyo.

Kadhalika Koka alisema kwamba katika kuboresha sekta ya afya wakati akiwa Mbunge alishatoa msaada wa vifaa tiba mbali mabli katika kituo cha afya ya Mkoani lengo ikiwa ni kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuhakikisha anasimamia vema suala zina la upatikanaji wa dawa ili wananchi waweze kupata matibabu bila usumbufu wowote.

Akizungumzia kuhusiana na suala la mipango yake katika kuboressha sekta ya  afya aliongeza kuwa anatambua bado kuna baadhi ya maeneo mengine kuna changamoto ya upatikanaji wa huduma ya aafya hivyo amewaomba wananachi waweze kumpatia ridhaa ya kuongoza katika kipindi kingine ili aweze kumalizia utekelezaji wa ilani ya chama katika kuwahudumia wananchi wote bila ya ubaguzi.

 

Kwa upande wake Mgombea  udiwani wa kata ya Maili moja kupitia tiketi ya ( CCM) Ramadhani Lutambi alisema kwamba  lengo lake kubwa ni  kuhakikisha  anasimama kidete katika kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya barabara pamoja na kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga na kukarabati  madarasa katika shule za msingi na sekondari.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi katika Halmashauri ya mji Kibaha Maulid Bundala alibainisha kwamba amewaomba wananchi kuhakikisha wanafanya maamuzi yaliyo sahii kwa  kuwachagua viongozi wanaotokana na CCM  wenye uwezo wa kusikiliza kero za wananchi na  kuleta maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Pages