October 02, 2020

Maembe: Nichagueni nitaipigania Bagamoyo


VITAL Maembe Mgombea Ubunge jimbo la Bagamoyo ,  amesema kuwa changamoto zisizokuwa na ukomo kwa  wananchi wa jimbo hilo  ndizo zilimpelekea kujitosa kwenye mbio hizo.

Akizungumza na wapiga kura wa jimbo hilo juzi tarehe 30 Septemba 2020, eneo la Mlingotini Bagamoyo , Maembe amesema kuwa wananchi wa jimbo  kuwa amechoshwa kuona bagamoyo haipati maendeleo ilhali ina kila sababu ya kuendelea.

Amesema kuwa Bagamoyo ni moja kati ya maeneo yenye kuvutia kwa uwekezaji wa utalii, kuwa bahari , ardhi yenye rutuba pamoja kuwa kama kitovu cha sanaa nchini.

Amesema kuwa atahakikisha biashara ya utalii, inarejea kwenye mji huo mkongwe uliobeba historia ya nchi ambayo itaongeza upatikanaji wa ajira.

“Nitasimamia uchumi wa watu wa bagamoyo kwa kuhakikisha watu wanavua bila kubugudhiwa Bahari ndio shamba letu haiwezekani tuzuiwe kulima”, amesema Maembe.

Amesema kuwa atakwenda bungeni kupigania marekebisho ya sheria ya uvuvi kwa kuwasilisha hoja mahususi  na kwamba pakiwepo  sheria mzuri wavuvi watanufaika.

Kuhusu suala la elimu amesema kuwa atapigania upatikanaji wa walimu , maabara,  na majengo pamoja na kujenga maktaba za kijamii katika kila Kata.

Kuhusu suala la Afya amesema kuwa atahakikisha Bagamoyo inakuwa na mradi wa kadi maalum ya matibabu ya dharura kwa magonjwa ya mlipuko na ajali kwa wakazi.

“Nitasimamia Afya  kwa mama na mtoto, kwa kuhakikisha kuwepo kwa zahanati za kutosha, vifaa tiba na dawa ili kupunguza vifo vya mama na mtoto” ameeleza Maembe huku akishangiliwa na wananchi “

Maembe ambaye ni Mwanaharakati anayetumia muziki, kuwasilisha utetezi wa hoja zake amesema akiwa mbunge wa jimbo hilo atasimamia utolewaji wa elimu ya sheria kwa wananchi ili kuepusha uvunjaji wa sheria  kupunguza uonevu pia kuwalirahisishia kazi Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment

Pages