October 06, 2020

MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM KASEKESE MPANDA

 

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana  na kuzungumza na Umati wa Wananchi wa Kijiji cha Ikaka, St. Maria na Kasekese Mpanda alipokuwa njiani akielekea Ikola Mpanda Mkoani  Katavi kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM leo Octoba 06,2020.

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Ikola Mpanda wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,  alipokuwa akuhutubia mkutano wa  kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM katika uwanja wa Ikola Stoo Mpanda Mkoani Katavi  leo Octoba 06,2020.

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa ndani ya ndege aina ya Helkopta 5Y-HSN ya Chama cha Mapinduzi CCM akijiangaa kuruka kutoka Kijiji cha  Ikola Mpanda Vijijini Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi kuelekea Mpanda Mjini baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Ikola  Jimbo la Mpanda Vijijini katika uwanja wa Ikola Stoo leo Octoba 06,2020.

No comments:

Post a Comment

Pages