MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohame Shein, akimnadi Dk. Hussein Mwinyi (kushoto), kupeperusha bendra ya CCM kwa nafsi ya Urais wa Zanzibar, na Issa Ussi Haji Gavu (kulia) kiwania nafasi ya Uwakilishi jimbo la Chwaka, wakati wa mkutano wa kampeni uliofnyika uwanja wa Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja.
WANACHAMA wa Chama
cha Mapinduzi CCM, walioshiriki katika mkutano wa kampeni za chama
hicho uliofanyika Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja
jana. (PICHA ZOTE NA ABDALLA OMAR).
jana. (PICHA ZOTE NA ABDALLA OMAR).
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR
MGOMBEA
Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Mwinyi amesema endapo
atapewa ridhaa ya kuwa rais,ataendeleza miradi yote iliyoasisiwa na
serikali ya awamu ya saba na kuanzisha miradi mipya ya kiuchumi.
Alisema serikali ya awamu ya saba imetekeleza Ilani kwa asilimia 90 katika sekta mbalimbali nchini.
Alisema
katika Ilani iliyopita wameanza ujenzi wa hospitali ya rufaa ya Binguni
katika wilaya hiyo na kwamba yeye atamalizia ujenzi huo.
Alisema katika utawala huo wamepandisha hadhi vituo vya Afya mbalimbali kwa lengo la kuboresha huduma za Afya nchini.
Alisema
katika sekta ya elimu Dk.shein,amejenga shule mbalimbali za ghorofa
katika Mkoa huo zenye vifaa vya kisasa vya kusomea na kufundishia masomo
yote.
Alisema pia zimejengwa barabara mbalimbali za kiwango cha lami katika Mkoa.
Aidha
Dk.Hussein,alisema serikali ya awamu ya saba wamefanikiwa kusambaza
maji kwa urefu wa kilomita 7.6 kutoka Bambi hadi Uroa.
Akizungumzia vipaumbe vyake alisema kuwa atamalizia miradi yote iliyoanzishwa na serikali ya awamu ya saba ambayo haikumaliza.
Alisema
atahakikisha anamaliza migogoro ya ardhi baina ya wananchi na
wawekezaji kwa kuweka utaratibu mpya wa kumiliki na kutumia ardhi.
Katika sekta ya maji safi na salama atahakikisha anaendelea kujenga miundombinu ya upatikanaji wa maji.
Aidha
kwa upande wa suala la mazingira alisema Kuna baadhi ya wananchi
wanatumia mistu kwa ajili ya kujipayia kipato hivyo kwa utawala wake
atahakikisha anawapatia kazi mbadala ili kunusuru mazingira
yasiharibiwe.
Alisema wajasiriamali wote watapewa mikopo,mafunzo,masoko na mitaji yenye fursa nafuu.
Alisema
ameahidi kutoa ajira kwa vijana ukiachilia mbali zile ajira 300,000
zilizotajwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025.
Pamoja na hayo alieleza kuwa patajengwa viwanda vidogovidogo na vikubwa kwa ajili ya kuongeza fursa za ajira.
Alisema
kupitia utekelezaji wa mpango wa uchumi wa bahati(blue economy),alisema
atahakikisha wavuvi wanapata vifaa vya kisasa vya uvuvi ili kwenda
sambamba na mabadiliko ya Mapinduzi ya kiuchumi nchini.
Kwa
upande wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,alisema wagombea wote walioteuliwa Wana uwezo na uzoefu wa
kukipigania Chama Cha Mapinduzi.
Alisema
viongozi hao sio wanagenzi katika medali za kisiasa na kiutendaji kwani
kila kiongozi ana uzoefu katika fani yake na majukumu wanayoomba kupewa
ridhaa na wananchi.
Alisema
viongozi hao watapewa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 ili
wakasimamie kwa uadilifu utekelezaji wake kwa kuwatumikia wananchi wote
bila ubaguzi.
Alisema
Dk.Mwinyi,ndiye aliyepewa dhana ya kupeperusha bendera ya CCM katika
kuwania kiti cha urais wa Zanzibar ambaye ni mgombea mwenye uzoefu
mkubwa kiutendaji.
Dk.Shein,aliwasihi
wananchi wamchague mgombea huyo wa CCM ili aendelee kulinda na
kudumisha Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na Muungano wa Serikali
mbili.
Akitaja sifa za
mgombea huyo wa kiti Cha Urais wa Zanzibar,Dk.Shein alisema kiongozi
huyo amehudumu ndani ya serikali kwa miaka mingi hivyo ana uzoefu mkubwa
katika masuala ya uongozi.
Alisema
kuwa Dk.Mwinyi, nafasi ya Urais anaiweza na ataongoza nchi kwa
mafanikio makubwa kwani amewahi kuhudumu katika Wizara ya Afya,amehudumu
katika Wizara ya masuala ya muungano na kushiriki katika vikao na
mijadala mbalimbali ya kuimarisha Muungano.
Akizungumzia
historia ya Zanzibar toka enzi za ASP kuwa uchaguzi wa pili wa Zanzibar
wa January 1961 Chama Cha ASP kilishinda kwa kura nyingi lakini
hakikupewa nchi na utawala wa wakati huo.
Alisema
kabla ya Mapinduzi wananchi waliishi maisha ya dhiki,tabu na mateso
makubwa huku wakikoseshwa haki zao za msingi kwa makusudi.
Makamu
Mwenyekiti huyo wa CCM,alieleza kuwa mateso dhidi ya wazawa ndio
yaliyochochea harakati za wananchi wa Zanzibar kutafuta njia ya
kujikombo kupitia Mapinduzi 1964.
Naye
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi,alisema CCM
imeendelea na kampeni zake chini ya mgombea wake Dk.Mwinyi ambaye
anawafuata wananchi wa makundi mbalimbali katika maeneo yake.
Aliwasisitiza
mabalozi wa mashina ya CCM kuwa ikifika Octoba 28,mwaka huu wahakikishe
wanapita nyumba kwa nyumba kuhamasisha wanachama na wananchi kwenda
kukipigia kuwa Chama Cha Mapinduzi.
Alisema
Wana CCM wahakikishe wanajitokeza kwenda kutekeleza matakwa ya Katiba
ya CCM ya mwaka 1977,ibara ya tano inayoelekeza kuwa ushindi wa CCM ni
lazima kwa kila uchaguzi.
"Wapo
baadhi ya viongozi wa kisiasa wameanza kuhamasisha vurugu na ubaguzi wa
kikabila na kidini jambo ambalo ni hatari kwa amani ya nchi na ustawi
wa maendeleo.
Vijana
msikubali kutumiwa na wanasiasa hao wasiokuwa wazalendo Kama wanaka
Octoba 27,mwaka huu kufanya vurugu basi waende wao wakapige hiyo kura ya
mapema lakini sio kuwahamasisha wananchi wasiokuwa na hatia kuvunja
sheria", alisema Dk.Mabodi na kuiongeza kuwa suala la kura ya mapema
lipo kisheria na watu wanaohusika na upigaji wa kura hiyo wanajulikana.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Unguja, Ramadhan Abdallah
Ali (Kichupa) alisema ndani ya Mkoa huo CCM ipo vizuri na wanasubiri
siku ya kupiga kura ili wakawachague kwa kura nyingi wagombea wote wa
chama hicho.
Akizungumza
kwa niaba ya wagombea uwakilishi wa wilaya ya Kati ,mgombea uwakilishi
wa Jimbo la Chwaka Issa Haji Ussi ,alisema uchaguzi uliopita CCM katika
jimbo hilo ilishinda zaidi ya asilimia 80 na mwaka huu wamejipanga
kushinda kwa zaidi ya asilimia 90.
Naye
mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo Haji Makame Mlenge alisema
kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda katika uchaguzi huo.
Anna Agata Msuya,amesema kuwa Zanzibar imepiga hatua kubwa kimaendeleo chini ya uongozi wa Dk.Ali Mohamed Shein.
Ameeleza
kwamba juhudi hizo za maendeleo zitakuwa na manufaa endapo wananchi wa
Zanzibar kwa pamoja wataamua kuwachagua wagombea wa CCM kuwa viongozi
kuongoza nchi.
Makamu
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Abdallah Haidar alieleza kuwa CCM
imeendelea kufanya siasa za kisitaarabu kwa kufanya kwa kina Sera zake
bila kutukana ama kubeza vyama vingine vya kisiasa.
Kwa
upande wake Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Maulid
Mwita,aliwaomba vijana bila kujali tofauti za kisiasa siku ya kupiga
kura wajitokeze kwa wingi kuwapigia kura wagombea wote wa CCM ili nchi
iendelee kupaa kiuchumi na kimaendeo.
Naye
Mjumbe wa Kamati ya siasa ya CCM ya Mkoa huo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa
kusini Unguja Ayoub Mahmoud Mohamed akifafanua utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 alisema wamefanikiwa kudumisha amani
na utulivu kwa kumaliza mgogoro wa vijiji vya Chwaka na Malumbi.
Pia alisema wamemaliza mgogoro wa vijiji vya Uzi na Ng'ambwa wananchi.
Alisema
katika sekta ya kilimo tayari zimetengwa hekta 892 kwa ajili ya kilimo
huku wakinunua mashine ya kusindika zao la ndimu kwa lengo la kuongeza
thamani zao hilo ili wananchi wanufaike na kilimo.
Ayoub,alisema katika Mkoa huo tayari wamekamilisha ramani ya ujenzi wa daraja la kutoka Unguja ukuu kwenda Uzi.
Pamoja
na hayo kwa upande wa sekta ya ufugaji alisema tayari serikali imenunua
mashine kwa ajili ya kusindika maziwa ili kuwaongezea thamani wafugaji.
No comments:
Post a Comment