Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 9, 2020, Katibu
Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa, alisema kuwa kuna ongezeko la
maombi kwa mwaka huu ukilinganisha na mwaka jana sambamba na uwingi wa
nafasi katika vyuo mbalimbali.
“Tume inasisitiza kuwa waombaji
ambao hawakuweza kutuma maombi kwa awamu ya kwanza na pia hawakudahiliwa
watumie nafasi hiyo kuomba kwenye vyuo wanavyovipenda”.
Akizungumzia
nafasi zilizopo kwa mwaka huu ni 157, 770 ikilinganishwa na nafasi 149,
809 kwa mwaka jana ongezeko ni nafasi 7, 961 za shahada ya kwanza sawa
na asilimia 5.3.
Kuhusu waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi kimoja kuthibitisha kimojawapo kuanzia oktoba 9 hado 17 mwama huu.
"Kwa
kupitia ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri uliotumwa kupitia namba
zao za siri au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili, "
"Wale
ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo wanashauriwa kuingia kwenye
mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe
mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitishia katika chuo
husika, " alisema Profesa Kihampa.
Aidha jumla ya programu 686 zimeruhusiwa kudahili ikilinganishwa na programu 645 kwa mwaka 2019/2020.
Profesa
Kihampa aliwataka walioomba pia kufanya uthibitisho wa udahili au
kuangalia orodha yao kwa waliopata chuo zaidi kimoja kupitia tovuti TCU
(www.tcu.go.tz).
October 10, 2020
TCU KUFUNGUA ZOEZI LA UDAHILI AWAMU YA PILI
TUME
ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufungua zoezi la udahili kwa
awamu ya pili ambapo itaanza rasmi Oktoba 12 hadi 18 mwaka huu.
Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Profesa Charles
Kihampa, akifafanua jambo jijini Dar es Salaam leo Oktoba 9, 2020 kuhusu kukamilika kwa Awamu
ya Kwanza na Kufunguliwa kwa awamu ya Pili ya Udahili wa Shahada ya Kwanza kwa
Mwaka wa Masomo 2020/21. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Udahili na Kanzi
Data, Kokuberwa Mollel na kKulia Mkaguzi wa Ndani, Lucy Mrikaria.
No comments:
Post a Comment