HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 10, 2020

TCU KUFUNGUA ZOEZI LA UDAHILI AWAMU YA PILI

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufungua zoezi la udahili kwa awamu ya pili ambapo itaanza rasmi Oktoba 12 hadi 18 mwaka huu.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 9, 2020, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa, alisema kuwa kuna ongezeko la maombi kwa mwaka huu ukilinganisha na mwaka jana sambamba na uwingi wa nafasi katika vyuo mbalimbali.

“Tume inasisitiza kuwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi kwa awamu ya kwanza na pia hawakudahiliwa watumie nafasi hiyo kuomba kwenye vyuo wanavyovipenda”.

Akizungumzia nafasi zilizopo kwa mwaka huu ni 157, 770 ikilinganishwa na nafasi 149, 809 kwa mwaka jana ongezeko ni nafasi 7, 961 za shahada ya kwanza sawa na asilimia 5.3.

Kuhusu waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi kimoja kuthibitisha kimojawapo kuanzia oktoba 9 hado 17 mwama huu.

"Kwa kupitia ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri uliotumwa kupitia namba zao za siri au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili, "

"Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitishia katika chuo husika, " alisema Profesa Kihampa.

Aidha jumla ya programu 686 zimeruhusiwa kudahili ikilinganishwa na programu 645 kwa mwaka 2019/2020.

Profesa Kihampa aliwataka walioomba  pia kufanya uthibitisho wa udahili au kuangalia orodha yao kwa waliopata chuo zaidi kimoja kupitia tovuti TCU (www.tcu.go.tz).

Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Charles Kihampa, akifafanua jambo jijini Dar es Salaam leo Oktoba 9, 2020 kuhusu kukamilika kwa Awamu ya Kwanza na Kufunguliwa kwa awamu ya Pili ya Udahili wa Shahada ya Kwanza kwa Mwaka wa Masomo 2020/21.
Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Profesa Charles Kihampa, akifafanua jambo jijini Dar es Salaam leo Oktoba 9, 2020 kuhusu kukamilika kwa Awamu ya Kwanza na Kufunguliwa kwa awamu ya Pili ya Udahili wa Shahada ya Kwanza kwa Mwaka wa Masomo 2020/21. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Udahili na Kanzi Data, Kokuberwa Mollel na kKulia Mkaguzi wa Ndani, Lucy Mrikaria.

No comments:

Post a Comment

Pages