HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 15, 2020

TFS YAHAMASISHA UTALII WA NDANI

Baadhi ya wadau wa utalii wakizunguka na mitumbwi katika bwawa la Minaki ambalo ni miongoni mwa vivutio vya utalii vinavyopatikana kwenye msitu wa Pugu.





Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeadhimisha kumbukizi ya baba wa taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwa kuhamasisha watanzania kufanya utalii wa ndani.


Akizungumza na kundi la vijana waliotembelea msitu wa Pugu Kazimzumbwi Ofisa misitu mkuu TFS kanda ya Mashariki Shaban Kiula amesema baba wa taifa anaswa kuenziwa kwa vitendo.


Alisema Mwalimu Nyerere alipenda utalii, maliasili na uhifadhi wa misitu hivyo ni vyema kuenzi vitu alivyovipigania kwa vitendo.


“Tumekuja kumuenzi hapa ili kutekeleza baadhi ya matamshi ambayo amewahi kuyatoa baba wa taifa. Ni muhimu kuendeleza vitu alivyovipigania,”

Kiula pia aliwasisitiza wadau wa utalii kuwekeza kwenye misitu ya asili ili kuvutia watalii wengi kuitembelea na kuongeza mapato.

Kwa  upande wake mshauri wa utalii, maliasila na mazingira wa mkoa wa Dar Mariam Kitula alisema suala la utalii si la serikali pekee kwani wananchi pia wanatakiwa kuwa sehemu ya rasilimali hiyo.


“Leo tunapomkumbuka Mwalimu Nyerere tuna kila sababu ya kuishi mawazo yake, kwake utalii na uhifadhi ilikuwa ni vitu alivyovipa kipaumbele.


“Tumuenzi kwa kuthamini na kulinda rasilimali zetu hizi ambazo ni vivutio vya asili kama misitu ya aina hii ambayo ukiacha kuwa kivutio ni inatuzalishia hewa safi,” amesema Kitula.

No comments:

Post a Comment

Pages