WATU wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa tuhuma za wizi wa fedha simu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 400,000.
Washtakiwa hao waliofikishwa mahakamani hapo ni Rajabu Hassan na Lukmani Juma ambao wamesomewa shtaka lao na Wakili wa Serikali Hamisi Saidi mbele ya Hakimu Mkazi Happiness Kikoga.
Akisoma shtaka hilo, Wakili Saidi amedai washtakiwa hao walitenda kosa hilo Julai 20, 2020, katika eneo la Kinondoni ambapo waliiba simu aina ya TECNO POP 1, yenye thamani ya shilingi 200,000 pamoja na fedha za kitanzania kiasi cha shillingi 220,000 mali ya Yuweni Jackson.
Amedai pia baada ya washtakiwa huyo kupokonya mali hizo walimjeruhi Jackson kwa silaha aina ya Panga .
Baada ya kusomewa shtaka hilo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na Hakimu Kikoga ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba, 19 mwaka huu ambapo kesi hiyo itakuja tena kwa ajili ya kutajwa.
No comments:
Post a Comment