November 21, 2020

Mikoa vinara kwa kutokuwa na vyoo bora yatajwa

MKURUGENZI wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Leonard Subi amesema kuwa mikoa ambayo bado ipo chini kwa ujenzi na matumizi ya vyoo bora ni Kigoma, Lindi, Dodoma na baadhi ya Kanda ya ziwa.

Aidha Dk. Subi amesema mikoa ambayo ni vinara kwa kuwa na vyoo bora ni Dar es Salaam, Iringa na Njombe.

Kutokana na takwimu hizo Dk. Subira amewataka watendaji kuanzia ngazi za mashina kuhamasisha ujenzi wa vyoo na kuhakikisha kila mwananchi anatumia choo bora.

Dk.Subi ametoa kauli hiyo jana jijini Dodoma wakati akizungumzana waandishi wa habari kuhusu siku ya matumizi ya choo duniani ambayo huadhimishwa Novemba 9 kila mwaka.

Amesema lengo ya siku hiyo ni kuikumbusha jamii kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za afya ikiwa ni hatua muhimu ya kujikinga na maradhi yanayoenezwa kwa njia ya uchafu.

“Wiki ya Usafi wa Mazingira mojawapo ya mikakati mahususi ambayo inatumika kuibua na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa usafi katika ustawi wa jamii hasa katika nyanja za afya, elimu, maji na uchumi lakini pia siku hii ina lengo la kuikumbusha jamii kutumia vyoo bora ili kujikinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza ya kiwemo ya kuhara, kuhara damu, kipindupindu na magonjwa ya minyoo ,”amesema na kuongeza kuwa

“Choo bora ni kile ambacho kina ukuta,Mlango, sakafu inayoweza kusafishwa ,kilichoezekwa vizuri na chenye sehemu ya kupumulia hewa ili kuondoa harufu ndani ya choo,”amesema

Aidha amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Zingatia usafi wa jinsia kwa usafi wa mazingira endelevu ‘ni kauli mbiu ambayo inaongeza umuhimu wa ujenzi wa vyoo bora kwa jamii na maeneo yote yenye mikusanyiko pamoja na kuweka mazingira katika hali ya usafi wakati wote.

Amesema matumizi ya vyoo bora ni afua muhimu katika kukinga na kudhibiti maradhi ya kuambukiza huku akisema asilimia 40 ya magonjwa
yanayosababishwa na uchafu.

No comments:

Post a Comment

Pages