Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema Tanzania itashirikiana na nchi yoyote duniani ambayo inatambua na kuheshimu Uhuru wa nchi na utu wa watu wake.
Prof.
Kabudi ametoa kauli hiyo jijini Dodoma alipozungumza na Watumishi wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na taasisi
zake tangu alipoteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.
"Tutafanya
kazi na nchi zote ambazo zinatuheshimu, zinatutambua kama Taifa huru,
kutuheshimu sisi kama binadamu wa mataifa mengine, hatutakubali
kudharauliwa, kutokuheshimiwa utu wetu na kudharauliwa kwa sababu ya
misaada au pesa’, amesema Prof. Kabudi
Ameongeza
kuwa Tanzania itasikiliza taifa lolote duniani na kujadiliana nalo kwa
heshima kwani mapungufu hayapo upande mmoja tu.
"Tuko
tayari kuwasikiliza na kujadiliana nao kwa heshima na kama wanadhani
kuna kitu kimepungua kwetu na sisi tunadhani kimepungua kwao," amesema
Prof. Kabudi.
Amesema Tanzania haiwezi kumruhusu mtu yeyote atumie misaada ya fedha kuondoa uhuru wetu na kutokuthamini utu wetu.
Amesema
Tanzania haiwezi kujitenga kama kisiwa na itaendelea kushiriki katika
shughuli mbalimbali za kidunia kama vile kulinda amani, kukabiliana na
mabadiliko ya hali ya hewa na kutunza mazingira.
"Hatutajitenga
katika dunia hii, tutaendelea kujumuika katika kazi mbalimbali kama
vile ulinzi wa amani, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na
kuhifadhi mazingira,’ alisema na kuongeza kuwa tumekuwa bandari ya amani
kwa wakimbizi sio tu kutoka Afrika bali duniani kote na tutaendelea
kuwa hivyo," Ameongeza Prof. Kabudi.
Prof.
kabudi pia amewataka watumishi wa Wizara kusoma kitabu cha Baba wa
Taifa Mwalimu Nyerere alichowaandikia watumishi wa wizara hiyo mwaka
1969 cha Usipayuke toa hoja ‘Don’t shout argue’ ili kutoa takwimu
sahihi kwa wakati.
Amesema
jukumu la kuieleza dunia kuhusu takwimu za vitu mbalimbali ni la
watumishi wa Mambo ya Nje na hawana budi kuhakikisha wanaliekeleza hilo
kwa ufasaha.
Mbali
na kitabu hicho, Prof. Kabudi amewakabidhi wakurugenzi wa Idara
mbalimbali Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hotuba za Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wakati
anafungu Bunge la 11 na hotuba ya ufunguzi wa Bunge la 12 na kuwataka
kusimamia na kutekeleza maagizo yote yaliyopo kwenye hotuba hizo pamoja
na maelekezo ya Ilani ya CCM.
Awali
akimkaribisha Waziri kuzungumza na watumishi, Katibu Mkuu Wizara Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wibert Ibuge aliwapongeza watumishi utendaji mzuri wa kazi na
kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uadilifu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)akimkabidhi nyaraka Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Balozi, Anisa Mbega |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)akimkabidhi nyaraka Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria Bibi. Caroline Chipeta. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)akiongea na Watumishi wa wizara katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma |
No comments:
Post a Comment