HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 13, 2020

Rais Magufuli aanza kuteuwa mawaziri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dk. John Pombe Magufuli leo tarehe 13 Novemba, 2020 amefanya uteuzi wa Mawaziri mawili katika Baraza jipya la Mawaziri.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Chamwino ilieleza kuwa Rais Magufuli amemteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Pili,  Rais Magufuli amemteua Dk. Philip Isdor Mpango  kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Mawaziri Wateule hao walikuwa wakishikilia nyadhifa hizo katika Baraza la Mawaziri lililopita na uteuzi huu unaanza leo tarehe 13 Novemba, 2020.

No comments:

Post a Comment

Pages