Majengo ya Shule ya Sekondari Mandarawe iliyopo Kijijini Nandenje
wilayani Ruangwa yanayojengwa na fedha za Usimamizi Shirikishi wa Misitu
ya Jamii (USMJ).
Mtendaji wa Kijiji
cha Nandenje, Rashid Najete akielezea waandishi wa habari namna dhana
ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu (USMJ) ulivyofanya mapinduzi kijijini
hapo.
Msimamizi na
Mtaalam wa Misitu wa Program ya Mnyororo wa Thamani ya Mazao ya Misitu
(FORVAC), Alex Njahani akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu program
hiyo.
NA SULEIMAN MSUYA, RUANGWA
KIJIJI
cha Nandenje, Kata ya Mandarawe, Wilayani Raangwa mkoani Lindi,
kimetumia zaidi ya shilingi milioni 279 zilizokusanywa kupitia dhana ya
Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (USMJ), kutekeleza miradi ya
kijamii na maendeleo.
Dhana
ya USMJ kijijini hapo imefikishwa na Shirika la Kuhifadhi Mpingo na
Maendeleo (MCDI) kupitia Program ya Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya
Misitu (FORVAC), inayotekelezwa n Idara ya Misitu na Nyuki chini ya
Serikali ya Tanzania na Finland.
Program
ya FORVAC inatelelezwa katika kongano tatu ambazo ni Tanga yenye wilaya
za Handeni, Kilindi, Mpwapwa na Kiteto, Ruvuma ni wilaya za Tunduru,
Nyasa, Mbinga na Songea na Lindi ni Ruangwa, Liwale na Nachingwea.
Kwa
mujibu wa Mtendaji wa Kijiji cha Nandenje Rashid Kajete amesema fedha
hizo zimekusamywa kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 baada ya wanakijiji
kupatiwa elimu na kutambua umuhimu wa USMJ kwenye vjjiji vyao.
Awali kijiji hakikuwa na uelewa kuhusu USMJ ila kila mtu ni mlinzi wa msitu kwani faida inaonekana.
Mtendaji
amesema fedha hizo zimefanikisha ujenzi wa Zahanati ya Nandenje kwa
zaidi ya shilingi milioni 49, nyumba ya mganga shilingi milioni 36, choo
cha zahanati shilingi milioni 4.3, kichomea taka shilingi milioni 8 na
kununua maeneo yanayozunguka zahanati kwa shilingi milioni 1.6.
"Ujenzi
wa nyumba walimu shilingi milioni 39, ukarabati nyumba za walimu
shilingi milioni 2, Shule ya Sekondari Mandarawe shilingi milioni 40,
ununuzi wa eneo la kujenga shule shilingi milioni 3.8," amesema Kajete.
Amesema fedha hizo zimetumika kununua trekta shilingi milioni 67.8, ujenzi wa jengo ka kuhifadhia trekta shilingi milioni 3.7 pamoja na ununuzi wa eneo la soko kwa shilingi 700,000.
Amesema mafanikio hayo yametokana na utekelezaji wa sera ya misitu ya mwaka 1998 inayotoa kipaumbele kwa jamii kushirikishwa katika usimamizi wa wa misitu kwa lengo kukuza kipato cha jamii ili kupunguza umaskini.
Amesema kupitia USMJ wanakijiji wekuwa na amani na upendo kwa kuwa hawabughudhiwi kwa kuombwa michango bali wanakaa kujadili matumizi ya fedha zinatokana na uvunaji endelevu wa misitu.
"Katika
kipindi hicho Halmashauri ya Ruangwa imekusanya zaidi ya shilingi
milioni 47.9 ambapo kamati ya misitu ya kijiji imekusanya zaidi ya
shilingi milioni 153 ni mafanikio makubwa.
Mtendaji
amesema kijiji kina watu wapatao 2,200 kwa mujibu wa sensa ya watu na
makazi ya mwaka 2012 na ukubwa wa hekta 12,745.48 na kwamba hekta 5025
ni hifadhi ya misitu ndio inachochea maendeleo hayo makubwa.
Kajete
ameongezea kuwa kijiji kina mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa ajili
ya kilimo, ufugaji na makazi ya watu hali ambayo imepunguza migogoro
baina yao.
Mtendaji amesema shilingi milioni 279 zepatikana baada ya kununwa miti michache ambayo ni Msekeseke, Mninga, Mtondolo, Mnangu na Mkongo huku misitu ukiwa salama.
Mjumbe wa Serikali ya kijiji hicho Juma Rashid amesema USMJ umeweza kuwakombo kiuchumi, kijamii na maendeleo hivyo watahakikisha misitu inakuwa salama.
Mtendaji amesema shilingi milioni 279 zepatikana baada ya kununwa miti michache ambayo ni Msekeseke, Mninga, Mtondolo, Mnangu na Mkongo huku misitu ukiwa salama.
Mjumbe wa Serikali ya kijiji hicho Juma Rashid amesema USMJ umeweza kuwakombo kiuchumi, kijamii na maendeleo hivyo watahakikisha misitu inakuwa salama.
Rashid
amesema kupitia miradi hiyo kuanzia mwakani watoto wao watatembea
umbali mdogo kwenda shule hivyo ufaulu utaongezeka na mimba za utotoni
zitapungua kama sio kuisha kabisa.
"Hayo aliyosema mtendaji ni ya kweli na sababu ya yote hayo ni misitu yetu ambayo tunaitunza kwa uendelevu," amesema.
Kwa
upande wake Salima Alli amesema kwa sasa ana amani kwani misitu
imesaidi kuwepo n jinsia kijijiji kwao kwa wanawake wengi kushiriki
kwenye maamuzi jambo ambalo awali halikuwepo.
Amesema kamati mbalimbali za kijiji zina wanawake ila ujasiri na usubutu umetokana na ushiriki wao kwenye USMJ.
Ofisa Misitu wa Wilaya ya Ruangwa James Kabuta amesema halmashauri hiyo inachukua asilimia 10 ya mapato yote ya mazao ya misitu kutoka kwenye Kijiji ambapo asilimia 60 inakwenda kijijini na asilimia 30 kamati ya misitu ya kijiji.
Amesema halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa uhifadhi ikiwemo FORVAC, MCDI, WWF, MJUMITA, CoFOREST na wengine wanaelekeza nguvu kubwa kwenye elimu kwani ndio mkombozi katika dhana ya. USMJ.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa, Mohamed Muhidin amesema
halmashauri itashirikiana na mdau yoyote ambayo atakuja na dhana
inayowezesha misitu kuwa endelevu kwa kuwa faida wanaiona kwenye vijiji
vya miradi kati ya vijiji zaidi ya 90 walivyo navyo.
Msimamizi
na Mtaalamu wa Misitu wa Program ya FORVAC,Alex Njahani amesema mradi
huo umegusa maisha ya watu zaidi ya 330,000 hivyo ni wazi kuwa ni mzuri
kiuhufadhi, kiuchumi na maendeleo.
Njahani amesema lengo la program ni kuona kila mwanajamii anayezungukwa na misitu ya jamii wananufaika na uhifadhi unaendelea.
"Tumenunua
mashine za kisasa za kuchakata mbao inayotembea (Mobile Sawmill) kwa
ajili ya mkoa wa Lindi na Ruvuma ambapo uzalishaji umeongezeka zaidi,"
amesema.
Njahani amewashauri wanavijiji kulinda na kuhifadhi misitu ili iwe endelevu kwa vizazi vya sasa na baadae.
No comments:
Post a Comment