TImu ya Mkoa wa Simiyu imeanza vema mashindano ya tenisi ya BQ baada ya wachezaji wake wote wanne kuingia hatua ya nusu.
Mashindano hayo yanayofanyika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam yakishirikisha watoto zaidi ya 125 kutoka mikoa zaidi ya mitano ambao wameonesha vipaji vya Hali ya juu.
Wachezaji wa Simiyu waliotinga nusu fainali ni Rebecca Kulwa, Rodha Joseph, Hellen Mtaka na Martha Mtaka.
Akizungumzia mafanikio ya TImu yake, Kocha wa TImu hiyo Mikidadi Bunaya, alisema yanatokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya wakipata sapoti kubwa ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka.
Michuano hiyo inatarajiwa kufikia tamati leo Novemba 29 kwenye viwanja hivyo.
No comments:
Post a Comment