Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohamed Said amesema kuna umuhimu mkubwa wa kufaya usafi wa mazingira katika maeneo yaliyowazunguka ili kujikinga na maradhi mbalimbali.
Akizungumza
wakati wa zoezi maalum la usafi wa mazingira kwa watendaji wote wa
Wizara ya Elimu Zanzibar amesema uwajibikaji kazini unahitaji mazingira
safi na salama.
Amesema
Wananchi wa Zanzibar wakiwa na utamaduni wa kuwa na siku maalum ya
kufanya usafi katika maeneo mbalimbali kutaisaidia nchi kua na miji
safi.
Aidha
amewapongeza watumishi wote wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar kwa kuitikia wito na kuhudhuria kwa wingi katika zoezi la usafi
ambalo limeleta muonekano mzuri katika wizara yao.
Amewataka kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakuwa endelevu ili kuweka mazingira safi na salama.
Nae
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu mu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt.Idrisa
Muslim Hija amesema ni muda wa wananchi wote wa Zanzibar kuendeleza
utamaduni wa usafi kwani usafi ni ibada katika dini zote.
Akizungumza
kwa niaba ya wafanyakazi wenzie wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar bi Nabila Habibu amempongeza Waziri wao kwa kuanzisha zoezi
hilo na kufanya Wizara yao kua mfano kwa Wizara yengine katika
kudumisha usafi maofisini.
Wakati
huo huo Mhe Simai ameshiriki usafi wa mzingira katika Taasisi ya
Sayansi Karume na kuwataka wanafunzi waliopo ndani ya dakhalia wa
Taasisi hiyo na kwengine kuhakikisha wanafanya usafi kila wiki ili
kujiepusha naradhi mbalimbali yakiwemo ya miripuko.
Kwa
upande wao Wanafunzi wa Dakhalia ya Taasisi ya Sayansi Karume KIST
wamekiri kuwepo kwa mazingira machafu ndani ya dakhalia yao ambapo
wameahidi kusafisha ili waondokane na muonekano mbaya wa dakhalia zao.
Katika
hatua nyengine zoezi kama hilo limefanyika katika ofisini mbalimbali za
Wizara ya Elimu Pemba ambapo Afisa Mdhamini wa Wizara hiyo Maalim
Mohammed Nassor ameliongoza hilo.
Zoezi
la usafi wa mazingira limefanyika katika Idara na Taasisi zote za
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar na litaendelea kufanyika
kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kuepusha ofisi kuwa na muonekano
mbaya.
No comments:
Post a Comment