Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), katika kuendeleza harakati za kupinga udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto nchini, kimeandaa mazoezi ya hiari ya siku moja ili kubadilisha tabia hasa za vijana dhidi ya fikra potofu za kubaka na kudhalilisha kwa ujumla.
Mazoezi hayo yatafanyika siku ya Jumamosi tarehe 28 kutoka Machomane hadi katika viwanja vya Gombani, Mkoa wa Kusini Pemba.
Hiyo
imekuja kutokana na kushamiri kwa vitendo vya udhalilishaji Zanzibar,
ambavyo vinafanywa zaidi na vijana wa kiume na makamo na kuharibu
mustakbali mzima wa maisha ya waathirika.
Mazoezi
hayo yataongozwa na Kikundi cha mazoezi cha Gombani pamoja na
kuhudhuriwa na vikundi vyengine vya mazoezi kama ni njia moja wapo ya
kuzuwia mihemuko kwa watu wenye tabia hiyo ovu ya ubakaji.
Hivyo,
kikundi cha Gombani kitatoa mazoezi ya aina tofauti kuwafundisha watu
wenye tabia za kubaka ili waweza kufanya mazoezi hayo mara kwa mara na
hivyo kuachana na fikra za ubakaji.
Shughuli
hiyo ni moja kati ya kazi za TAMWAZNZ na wadau katika kipindi hichi cha
siku 16 za kupinga udhalilishaji zilizoanza tarehe 25 mwezi huu na
kumalizikia tarehe 10 Disemba.
Shughuli hiyo muhimu inaambatana na ujumbe wa kitaifa mwaka huu ‘Tupinge
Ukatili wa Kijinsia: Mabadiliko Yanaanza na Mimi’ sambamba na ujumbe maalumu wa TAMWA ZNZ. ‘Fanya mazoezi zuia mihemuko: Muache mtoto wakike salama’
Aidha shughuli hiyo inategemewa kuwakutanisha wadau wa kupinga udhalilishaji kujadili hali na mwenendo wa vitendo hivyo Zanzibar ikiwa ni pamoja na kutafakari mbinu na hatua za kuchukuliwa zaidi ili kukabili na vitendo hivyo.
Zaidi ya wadau 300 wanategemewa kushirik katika maadhimo hayo wakiwemo taasisi za kijamii na za kiserikali.
TAMWA
ZNZ inaiomba jamii kuitumia siku hii kama kichocheo cha kubadili
tabia na kujenga utaratibu wa kushiriki ufanyaji wa mazoezi mara kwa mara ili kujikinga na maradhi nyemelezi pamoja na kujiepusha na uwezekano wa vishawishi hatarishi vinavyopelekea kuchochea kutekeleza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.
No comments:
Post a Comment