Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa kesho Novemba 24 mwaka huu.
Mvua hiyo yenye uwezekano wa wastani, itanyeeshaa kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani vikiwemo visiwa vya Mafia na Lindi.
Kwa mujibu wa taarifa ya TMA iliyoyolewa leo Novemba 23, 2020 imeonesha kwamba kesho Novemba 24, mvua kubwa itanyesua kwenye baadhi ya mikoa hiyo.
Taarifa hiyo inayoelezea hali ya hewa kwa siku tano kuanzia Novemba 23 imeonesha kuwepo kwa hali ya kawaida ya hewa kwa siku nyingine isipokuwa kesho.
“Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji jambo linaloweza kuathiri shughuli za kiuchumi huku ikiwataka wananchi kuzingatia angalizo hilo,” ilisomeka hivyo sehemu ya taarifa ya TMA.
No comments:
Post a Comment