Lakini,
mtaalamu bingwa kutoka *Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI),
Profesa Mohamed Janabi,* ana kidokezo kuhusiana na matumizi ya nadharia
hiyo kiholela kwamba yanaweza kumrudisha mhusika katika maradhi zaidi.
Profesa
Janabi, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo anasema maji
hayo ya ziada yanakuwa na manufaa kwa mnywaji iwapo tu kuna kiwango
sahihi cha kuushughulisha mwili wake hata maji hayo yakatumika kwa
manufaa kiafya.
Kwa
mujibu wa Profesa Janabi, katika hali ya kawaida, mwili wa binadamu huwa
na kiwango cha wastani wa lita tano za maji zinazokuwa kwenye mzunguko
mwilini na panapotokea maji ya ziada pasipo kutumika, ni hali
inayouchosha moyo na kuishia katika kuzalisha maradhi.
Mtaalamu
huyo anafafanua kwamba mwili wa binadamu unapokosa shughuli ngumu
zinazosababisha jasho kutoka, kiwango cha juu cha unywaji maji kinapaswa
kisizidi kati ya lita moja na nusu hadi mbili kwa siku.
“Maji
yanayohitajika kwenye mwili wa binadamu kwa siku ni lita moja na nusu,
kama hamna joto wala hufanyi kazi ngumu, unasababisha hatari kwenye moyo
wako.
“Mzunguko wa damu
tayari una lita tano na wewe unakunywa lita tano, kwa hiyo unaulazimisha
moyo kusukuma mara mbili zaidi na mwisho wa siku unajikuta una shida ya
moyo,” anatahadharisha.
Profesa
Janabi anaeleza kwamba, wakati moyo wa mtu unafanya ya kusukuma maji ya
ziada kuliko uwezo wake, athari inayofuata baada ya hapo ni baadhi ya
chembe hai muhimu zinaanza kufa moja baada ya nyingine zikipishana na
maradhi kuanza kuchukua nafasi yake.
Bingwa
huyo wa maradhi ya moyo, alitoa katika hadhira ya kilele cha
maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani, Septemba 29 mwaka huu katika
Viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.
Mtalaamu
huyo anaelekeza kidole cha tahadhari hasa kwa watendaji wa maofisini na
mazingira yanayofanana nayo kwamba mbali na hatari ya kuuchosha moyo,
pia ziada ya maji hayo imebeba hatari kuyeyusha madini muhimu kwa mwili
wa binadamu.
*ULAJI NAO TATIZO*
Profesa
Janabi anataja sababu nyingine kubwa ambayo watu hawafahamu kama ni
chanzo cha kuugua maradhi ya moyo kuwa ni ulaji usio wa mpangilio.
Anasema
ulaji wa vyakula vya mafuta umekuwa ukitajwa na wengi kuwa tatizo kubwa
katika kusababisha maradhi ya moyo, lakini siyo chanzo wala tatizo
kubwa bali *Ulaji wa vyakula vya wanga ndiyo mzizi wa tatizo.*
Anasema
vyakula vya wanga kama *Ugali na We* vinavyoliwa mara nyingi na
Watanzania huhatarisha usalama wa moyo na hivyo *Anashauri* watu
*kupunguza* ulaji wa aina hiyo ya vyakula.
*“Ukiweza
kujibana, basi unaweza kupunguza kula ugali na wali angalau ule mara
mbili kwa wiki kwa vyakula hivi,”* anashauri Profesa Janabi.
Anasema ratiba ya vyakula hivyo pia ni lazima izingatiwe na walaji kwa usalama wa moyo.
*“Mtu
anakula saa tatu, nne hadi saa sita usiku sahani kubwa ya wali au
ugali, akimaliza hapo anaingia kitandani analala, hapo badala ya chakula
kufanya kazi kinaenda kukaa kwenye stoo,”* anatahadharisha Profesa
Janabi.
Anasema
mlundikano huo ndiyo husababisha zaidi madhara kwa mwili wa binadamu
kama vile kutengeneza vitambi, shinikizo la damu na matatizo ya moyo.
Profesa
Janabi anashauri kuwa muda sahihi wa kula chakula ni kuanzia saa 12
jioni hadi saa 1:00 usiku, ikiwa ni saa chache kabla ya kwenda kulala.
*HALI ILIVYO KITAIFA*
Profesa
Janabi anasema magonjwa ya moyo huchangia karibu asilimia 31 ya vifo
vyote duniani na kwamba takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO)
zinabainisha kuwa kila mwaka, takribani watu milioni 18 hufariki dunia
kutokana na maradhi hayo.
“Ni
tatizo linaloonekana kuongezeka, takwimu zinaonyesha katika kila
wanawake wanne na wanaume watano, mmoja ananakabiliwa na tatizo la
shinikizo la damu,” anabainisha.
Anaongeza
kuwa magonjwa ya moyo ni kati ya magonjwa yasiyoambukiza, ambayo kinga
ni rahisi kuliko tiba, ndiyo maana WHO pamoja na Jumuiya ya Magonjwa ya
Moyo Duniani baada ya kuona yanaongezeka, wakaamua kuanzisha Siku ya
Moyo Duniani.
"Watu pia
wanapaswa kuzingatia unywaji wa pombe kwa kiasi, kuacha uvutaji wa
sigara, kula vyakula vinavyofaa, wazingatie kunywa dawa wanazoandikiwa
(waliokutwa na matatizo haya) na wafanye mazoezi, wapunguze uzito
uliopitiliza. Haya ni mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wa mtu bila
gharama,” anasema.
Mkurugenzi
huyo anabainisha kuwa JKCI tangu mwaka 2015 ilipoanzishwa hadi sasa,
tayari imeshaona takribani wagonjwa 350,000 huku 6,000 kati yao
wakifanyiwa upasuaji.
“JKCI tupo mstari wa mbele kutoa elimu ili watu waepuke magonjwa haya,” anasema Profesa Janabi.
BP IKO JIRANI
Mtaalamu huyo anabainisha kuwa asilimia 70 ya wagonjwa wanaotibiwa JKCI, wanakabiliwa na tatizo la Shinikizo la Damu (BP).
Anasema
takwimu zao zinaonyesha ndiyo tatizo linaloongoza kwa idadi kubwa ya
wagonjwa katika taasisi hiyo tangu ilipoanzishwa rasmi mwaka 2015.
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa JKCI, Samweli Rweyemamu, anasema wapo pia
wengine wanaokabiliwa na tatizo la kuziba kwa mishipa ya damu
inayosambaza damu kwenye moyo ambayo husababisha kifua kuuma.
“Kuna
wengine wanaohitaji upasuaji na idadi inaongezeka kila siku. Kwa mfano,
wale ambao mishipa ya damu inaziba, tunawazibua kwa upasuaji mkubwa au
ule wa tundu dogo,” anasema Dk. Rweyemamu.
Anabainisha
kuwa hadi Desemba mwaka jana, waliwachunguza karibu wagonjwa 1,000,
ambao awali walikuwa wakipewa rufani ya kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Daktari
bingwa huyo anasema kuwa kwa siku, huwa wanaona wagonjwa kati ya 300 na
400, hali inayoonyesha kwamba watu wenye matatizo ya moyo wanaongezeka
nchini.
Dk. Rweyemamu
anatoa mfano I got kwamba Wilaya ya Temeke kwenye Viwanja vya Zakheem
walipima watu 100 na kati yao, asilimia 18 walikuwa na BP IS na wengine
moyo umetanuka. Pia, 21 walionekana wana matatizo ya moyo.
Anasema
pia walifanya kazi kama hiyo katika viwanja vya Mwembe Yanga kwa watu
150 na kati yao, asilimia 22 walionekana kuwa na maradhi ya moyo.
Anasema kati ya hiyo asilimia 22, asilimia 19 walikuwa na shinikizo la
damu la juu.
Anaongeza
kuwa idadi hiyo inawezekana kuwa ni ndogo lakini utafiti uliofanyika Dar
es Salaam, unaonyesha karibu asilimia 30 wana shida ya shinikizo la
damu.
“Sasa ukiwa na
shinikizo la damu ni ‘risk factor’ (ishara hatari) ya kuziba kwa mishipa
ya moyo hatimaye utafika kwetu tukuzibue kwa vifaa maalum,” anasema Dk.
Rweyemamu.
Anasema mtu
akiwa na shinikizo la damu, moyo hutanuka na kuwa na dalili za kushindwa
kufanya kazi, hivyo asilimia kubwa ya matatizo ya moyo kwa watu wazima
yanaanza na presha.
Mratibu
wa Tiba wa Manispaa ya Kinondoni kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa
Manispaa hiyo, Dk. Omary Mwangaza, anasema kipindi cha Julai na Agosti
mwaka huu, katika vituo vya kutolea huduma za afya, waliibua wagonjwa
wapya zaidi ya 600 wanaokabiliwa na magonjwa yasiyoambukiza.
“Shinikizo
la damu na kisukari ni magonjwa yaliyokuwa yakiongoza kwa idadi kubwa
ya wagonjwa, wagonjwa wote hawa tumewaingiza kwenye mfumo wetu wa
matibabu,” anabainisha.
No comments:
Post a Comment