Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB), Imani Sichalwe, akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Kibaha Mkoani Pwani kwa ajili ya kutembelea baadhi ya viwanda vya kuchakata nyama pamoja na kujionea shughuli mbali mbali wanazozifanya wafugaji.
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Uongozi wa bodi ya nyama Tanzania (TMB) umesema kwamba utahakikisha unaendelea kushirikiana bega kwa began a wawekezaji wa viwanda kwa lengo la kuweza kuwaondolea changamoto zao mbali mbali zinazowakabili ikiwemo suala la vibali maalummu kwa ajili ya kuuza nyama zao katika nchi za njkuingilia kati kwa kulivalia njugaS Sakata la kunyimwa vibali kwa ajili ya kuuza nyama katika nchi za nje ili kutimiza malengo waliyojiwekea.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Imani Sichalwe wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Kibaha yenye lengo la kutembelea baadhi ya maeneo ikiwemo viwanda ili kuweza kujionea shughuli mbali mbali zinazofanyika pamoja na kubaini changamoto zilizopo ili kuweza kuzichua na kuzitafutia ufumbuzi.
Pia Kaimu huyo alibainisha kuwa kwamba kwa sasa wameshaanza mipango ya kuzungumza na baadhi ya mabalozi wa nchi husika hususan za Uharabuni ili kuona namna ya kuweza kupata vibali na kuwasaidia wafugaji waweze kupata soka la uhakik ambalo litawafanya wafugaji pamoja na wawekezaji kuuza nyama yao bila usumbufu wowote ule.
“Kwa kweli kitu kikubwa ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuweka mipango ya kuzungumza na mabalozi wan chi husika ambao wana mahitaji ya kupata nyama kutoka Tanzania hususan katika nchi za uarabuni na mchakato huu tayari tumeshaunza na kwamba mazungumzo pindi yakikamilika yataweza kuwa mkombozi mkubwa kwa viwanda ambavyo vinachakata nyama kupata soko la uhakika,”alifafannua Msajili huyo.
Katika hatua nyingine aliongeza kuwa lengo lao kubwa ni kuendekea kutoa elimu ya kutosha kwa wafugaji mbali mbali nchi nzima juu ya umuhimu wa kuzingatia maelekezo mabyo yanatolewa na wataalamu wa mifugo kwa ajili ya kuweza kuhudumia ipasavyo ikiwemo kuwapatia chanjo ili kuondokana na changamoto ya mlipuko wa magonjwa.
“Kitu kikubwa ni kuhakikisha kwamba tunawaondolea wawekezaji wetu wa ndani na wale wan je ya nchi changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa zikiwakabili na kupelekea wakati mwingine kukwamisha malengo waliyojiwekea katika kukuza uchumi wa nchi na kuunga mkono juhudi za serikali katika kuchangia pato la Taifa kupitia sekta ya viwanda,”alifafanua .
Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijiji Michael Mwakamo amebainisha kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utakuwa ni mkombozi mkubwa katika suala zima la kukuza uchumi pamoja na kuwapatia vijana fursa za ajira na kuondokana na wimbi la umasikini.
Pia Mwakamo alimpongeza Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kuweza kuhimiza ujenzi wa viwanda mbali mbali ambavyo vimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wan chi pamoja na kutoa fursa za ajira kwa vijana wengi ambao wameweza kunufainika katika suala zima la kujikwamua na wimbi la umasikini.
No comments:
Post a Comment